Na
Father Kidevu Blog, Arusha
HATIMAYE Askofu Stanley
Hotay ameapishwa rasmi kuwa Askofu wa Dayosisi ya Mount Kilimanjaro (DMK),
baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kuifuta kesi iliyokuwa inapinga kuapishwa
kwake.
Kesi hiyo ilifunguliwa na
waumini watatu wa Kanisa hilo ambao ni Looti Oilefu, Godfrey Muhone na
Frank Jacob.
Akizungumza katika Ibada
ya kumuapisha na kumuweka kitini Askofu Hotay, Askofu Mkuu wa Kanisa la
Anglikana Tanzania, Askofu Dk. Valentino Mokiwa kwanza alipongeza Mahakama kwa
kumpa Kristo Yesu haki yake.
Mbali na kuipongeza
Mahakama Kuu Askofu Mokiwa alimpongeza Jaji Fatuma Masengi kwa kutoa hukumu
iliyoleta heshina na amani ndani ya Kanisa.
“Ninamshukuru Mungu kwa
Jaji kutoa hukumu hii, Mungu amuongezee siku za kuishi na Mungu amlinde kama
Rais Jakaya Kikwete ananiskia alipo namuomba amuongezee cheo,”alisema Askofu
Mokiwa.
Hata hivyo akizungumzia
kuhusu hatima ya waumini hao na mtazamo wa washirika Askofu Mokiwa alitangaza
msimamo wa kuwasamehe na kuwataka kurejea kundini kuendelea kufanya kazi ya
Mungu.
Kwa upande wake Askofu
mpya Hotay akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Magessa Mulungo, alianza kwa kumshukuru Mungu kwa uamuzi uliotolewa na Mahakama
Kuu ya Tanzania.
"Ninafsi natangaza
kuwasamehe kwani walikuwa hawajui walitendalo ndani ya Kanisa la Kristo
Yesu," alisema Askofu Hotay.
Naye mgeni rasmi katika
Iabada hiyo RC Mullongo alijikuta akigeuka muhibisi na kuwaeleza waumini hao
kwamba hakika Yesu Kristo ameshinda.
“Hili tukio la kuapishwa
kwa Askofu Hotay Serikali tunaliheshimu sana, tumepata faraja kubwa kwani kama
msingetanguliza amani leo haki mliyopata mahakamani msingeiona haki ya leo.
“Mliendelea kuwa watulivu
hakumfanya maandamano mlikaa kimya na kumtanguliza Mungu. Lakini wapo wapo
wanaojidanganya eti ni lazima uvuruge amani ili upate haki wakati si kweli.
“Sasa leo nimekuja hapa
kuwauliza tunagombea nini, kinachofanya tutangaze nje kwamba hatuelewani ni
nini? Kwangu mimi huo ni uroho tu. Ndani ya Serikali tunasema Askofu Hotay
unastahili na tutakunga mkono,” alisema Mulongo.
Akizungumzia kuhusu
umuhimu wa kutanguliza maadili na nidhamu kwa viongozi wa dini, Mulongo
alibainisha kuwa Taifa ambalo wananchi wake wameandaliwa vizuri kiroho siku
zote huwa inakuwa kazi rahisi kwa Serikali iliyopo kufanya kazi zake kwa amani.
Wiki iliyopita Mahakama
Kuu Kanda ya Arusha iliyatupilia mbali maombi yalifunguliwa na waumini watatu
wa Dayosisi hiyo wakidai Askofu Hotay hakuwa na sifa za kuchaguliwa.
Hata hivyo katika uamuzi
uliotolewa na Jaji Masengi alidai walalamikaji katika shauri hilo hawakuwa na
hoja za msingi za kupeleka shauri hilo mahakamani badala ya kulipeleka kwenye
ngazi na taratibu za Kanisa kwani Kanisa hilo linayo Katiba yake inayoliongoza.
Kufutwa kwa kesi hiyo
sasa kulitoa nafas ya kukamilisha baadhi ya taratibu za Kiangalikana ambazo
hazikufanyika katika kumkabidhi Askofu Hotay Dayosisi ikiwamo kula kiapo na
kukalishwa kitini.
No comments:
Post a Comment