Na Mbaruku Yusuph,
Tanga
MAAFANDE
wa Mgambo Shooting watakaoshiriki kwa mara ya kwanza Ligi Kuu ya Bara, kesho
watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar, kwenye Uwanja wa Mkwakwani
jijini hapa.
Wakati
Mgambo wakitarajiwa kucheza kwa mara ya kwanza ligi hiyo iliyopangwa kuanza
Septemba 15, Mtibwa chini ya kocha wake Mecky Maxime, ni mabingwa mara mbili
1999 na 2000.
Akizungumza
jijini hapa jana, Meneja wa Mgambo Shooting, Dennis Mwingira, alisema maandalizi
ya mechi hiyo yanaendelea vizuri na kila kitu kimekamilika.
Mwingira
alisema mechi hiyo itakuwa ni maandalizi ya timu hiyo kujiandaa na Ligi Kuu
ambapo wataanza kampeni yao dhidi ya Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’ kwenye
dimba la Mkwakwani hapo Septemba 15.
Alisema
katika mechi hiyo ya ufunguzi watahakikisha wanapambana kufa au kupona kuchukua
pointi tatu kutoka kwa Coastal Union.
Mwingira
alisema wanasikitishwa na majeruhi waliyokuwa nao, ambao wametokana na michuano
ya Majeshi iliyojulikana kama ‘Sita bora teule’ iliyofanyika Kibaha mkoani
Pwani, ingawaje watajipanga kukabiliana na hali hiyo.
Chanzo: Tanzania
Daima
No comments:
Post a Comment