Msafara
maarufu duniani unaojulikana kama 'Annual animal Migration' unaohusisha wanyama
aina ya Nyumbu umeanza kurejea katika makazi yao ya Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti wakitokea mapumziko ya mwezi mmoja katika nchi ya jirani ya Kenya,
hususan kwenye mbuya ya Masai Mara.
Kila
mwaka, nyumbu pamoja na wanyama wengine kama pundamilia na swala hufanya
mzunguko maalum unaochukua miezi 12 ya mwaka ambapo miezi kumi kati ya hiyo
huwepo nchini katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na iliyobaki hutumiwa na
wanyama hao katika eneo la Hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya.
Mwaka
huu msafara huu unaohusisha wanyama zaidi ya Milioni Moja na Nusu na ambao
hutembea katika mzunguko wa takribani Kilometa 1,000 umewahi sana kurejea
nchini ukitokea mapumziko. Kwa mujibu wa taarifa za kitaalamu hali hii
inatokana na kuwahi kunyesha kwa mvua katika eneo la Serengeti ambapo
imesababisha kuwepo na nyasi nzuri ambazo ni chakula muhimu kwa wanayama hawa.
Changamoto
kubwa wanayokutana nayo msafara huu mara unaporejea nyumbani ni tukio la kuvuka
Mto Mara ambao umejaa wanyama wakali aina ya mamba na viboko ambao nao huwa ni
msimu wao wa kujipatia chakula kwa kuvizia na hatimaye kuwakamata wanyama hawa
mara wanapovuka mto. Watalii kutoka maeneo mbalimbali duniani wamekuwa
wakifurika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kushuhudia tukio hili adimu la
kuvuka Mto Mara ambalo wengi wao wamekuwa wakiliona kupitia filamu mbalimbali
zilizotengenezwa katika eneo hili.
No comments:
Post a Comment