Na Walter Mguluchuma - Mpanda- Katavi.
Dreva wa kampuni ya mabasi ya Air busi inayo fanya safari zake kutoka Tabora kuelekea Mpanda mkoa wa Katavi Nasibu Ramadhani (33) anashikiliwa na jeshil la polisi wilayani hapa kwa tuhuma za kukutwa na mwanafunzi wa kike (13) usiku akiwa amelala nae kitanda kimoja kwenye nyumba ya kulala wageni.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa hapo jana majira ya saa 6 usiku katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Miami iliyoko katika mtaa wa majengo wakati polisi walipo kuwa wakifanya doria kwenye nyumba za kulala wageni.
Baada ya Nasibu kuamshwa na mhudumu wa gesti hiyo ambaye alikuwa ameambatana na polisi na ndipo alipo ufungua mlango wa chumba walicho kuwa wamelala la msichana huyo.
Baada ya kuingia ndani ya chumba hicho polisi walishikwa na butwa kwa jinsi msichana huyo alivyo kuwa na umri mdogo na alivyo weza kuwa kwenye maeneo hayo na mwanaume kwenye nyumba ya kulala wageni.
Hari hiyo iliwafanya polisi wamfanyie maojiano msichana huyo ambaye alieleza kuwa yeye ni mkazi wa kijiji cha Tutuo mkoani Tabora wazazi wake walimkabidhi dreva Nasibu ili aweze kusafiri nae na amfikishe tarafa ya Inyonga wilayani Mlele mkoa wa Katavi ambapo angepokelewa na ndugu zake.
Hata hivyo baada ya kufika Inyonga Nasibu alimpitiliza msichana huyo hadi wilayani Mpanda na kumfikishia moja kwa moja kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni.
Msichana huyo alieleza kuwa baada ya kumfikishia hapo alimlazimisha walale wote na ndipo alipo weza kumkatalia alimlazimisha na kumpiga makofi na ndipo aliweza kuzidiwa nguvu.
Alieleza hari hiyo ilimfanya akubaliane na alicho kuwa akikitaka dreva huyo kwa kuhofia usalama wake na pia kutokana na kutokuwa na mwenyeji yoyote mjini Mpanda
Katika maelezo yake aliyo yatowa Nasibu kwa jeshi la polisi alieleza kuwa ilimlazimu ampitilize msichana huyo baada ya kutowakuta ndugu wa msichana huya katika kituo cha Inyonga.
Jeshi la polisi wilayani hapa limethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa na tayari taratibu za uchunguzi wa kidakitari zimeanza kumfanyia uchunguzu msichana huyo.
No comments:
Post a Comment