BM BARBERSHOP KINONDONI

Saturday, November 3, 2012

MENEJA WA MSAMA JIMMY CHARLES ACHANA NA MAISHA YA KULA CHIPS KAVU

Ushahidi wa Milele
Katika Kitabu kitakatifu cha Mungu Biblia Bwana Yesu alisema Mtu ataachana na Wazazi wake na kuungana na Mwenzake na hapo watakuwa mwili mmoja. Hakika ukiwa Mkristo wa dhehebu lolote lile utakuwa mkamilifu kama utatimiza nguzo au maagano matatifu ambayo wakristo huyaita maagano ambayo ni KUZALIWA, UBATIZO, KIPAIMARA, NDOA na KIFO. 

Bwana Jimmy Charles na Bi. Janet Christopher siku ya tarehe 27/10/2012 walitimiza agano hili takatifu la NDOA katika Kanisa la KKKT Usharika wa Kipawa na kuhudhuliwa na mamia ya watu na baadaye kwenye sherehe maalum maeneo ya nyumbani kwa bwana harusi Kawe Mlalakuwa Jijini Dar es Salaam. Kurunzi ya Mwanatanga ilimnasa Mkurugenzi Mtendani wa Msama Promotions ambye ndiye Mmiliki wa Makampuni Tanzu ya Msama bwana Alex Msama Mwitta ambaye alionekana kuwa na furaha kubwa baada ya Kijana wake Jimmy kuachana na maisha ya kula Chips Kavu kwa EDDI BABA pale Kinondoni Kanisani.

Jimmy na Janet au THE JJ wanasema VICHENCHEDE KAENI MBALI WAO NIWAMOJA SASA.

Tendo la kuonyesha kuungana (PETE) Kunako Kidole
Mkurugenzi Mtendaji akiwapongeza Maharusi
Bwana Harusi Jimmy Charles akiwa na Bestman wake  wakati wa Harusi hiyo
Mapacha wa NDOA bwana na Bibi Harusi ambao majina yao sasa ni Mr. & Mrs. Jimmy 

No comments:

Post a Comment