Sabrina Pazzy tako Mbetembete akiwa na Asha Sharapova Shoga yake mkubwa na mpinzani wake Kikazi. |
Akiongea na Kurunzi ya Mwanatanga Sabrina alitanabahisha kuwa ameondoka Mapacha kwasababu binafsi na ameaga na kupata busara za Wakurugenzi wa Band kwakuwa miziki ni Furaha na Miziki ni Burudani na si uadui. Namnukuu " Niliondoka Twanga kwa ridhaa yangu kwenda kutafuta maisha na kubadilisha upepo, lakini nimekaa chini na kusoma alama za nyakati nikaona sina future ndani ya Mapacha hivyo nimeona bora nirejee kwa Mama yangu Asha Baraka Mlezi wa Wana. Nimeomba idhini kwa viongozi wa Band ya Mapacha wamenikubalia japo kwa shingo upande lakini kwakuwa nilishaamua kwa sababu ya maslahi ya maisha na kipaji changu nimeamua kujiunga na bendi yangu mama na ninajua huku nitapata changamoto ya kikazi na kimaisha pia.
Kurunzi iliongea na Meneja wa Mapacha Watatu "Hamic Dacota" ambaye siku za karibuni amepata kazi kwenye Kiyuo cha DTV kwenye Kipindi cha X-Africa na haya ni maneno yake. "Tumemruhusu Sabrina Pazzy kwa moyo Mkunjufu kwenda Twanga Pepeta, hatuna neno la zaidi la kuongezea zaidi ya kumtakia kila la kheri kwakuwa miziki ya kibongo hivyo ndivyo ilivyo.
Mbetembete akikamua sambamba na Kiongozi wa Band - Salehe Kupaza (SACOSS) |
Kwa upande wa Management ya ASET kupitia Meneja Hassan Rehani ameidhibitishia Mwanatanga kuwa tayari Sabrina ameshaingia Mkataba wa kuitumikia ASET na leo atatamburishwa rasmi kwa wadau wa Twanga pale Billicanas, Maisha Club, Mango ili kupata baraka za wadau kwakuwa Twanga ni Bendi ya Jamii.
Sabrina akisaini Posho ya Mazoezi akiwa na Sharapova |
No comments:
Post a Comment