Viwanja vya Mahakama ya Kisutu leo vilitawaliwa na Nderemo Vifijo na vilio baada ya hukumu ya Uhujumu uchumi iliyokuwa ikimkabili Balozi Profesa Costa Mahalu kutangazwa kuwa ameshinda. Taarifa zaidi juu ya Hukumu hiyo italetwa kwa wasomaji wa mwanatanga blog siku si nyingi. Fuatilia matukio ya Hukumu hiyo kwa picha.
|
Waandishi wa habari
wakimfuata Balozi Profesa Mahalu akiwa pamoja na Mdogo wake Mirasi Rama
wakitoka nje ya Mahakama ya Kisutu Mchana huu mara baada ya kushinda kesi
iliyokuwa ikimkabili akidaiwa kununua nyumba ya Ubalozi wa Tanzania nchini
Italia, Akisoma hukumu iliyosomwa kuanzia Saa sita leo na Hakimu Mfawidhi mkazi
wa mahakama ya Kisutu Mh. Ilivin Mugeta imemtoa Balozi Profesa Mahalu katika
hatia na kumwachia huru
|
|
Mmoja
wa washitakiwa aliyeshitakiwa pamoja na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini
Italia, Profesa Costa Mahalu, Grace Martine (katikati), akisaidiwa na ndugu
zake kutoka Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam leo, baada ya kushinda kesi yao
ya kuhujumu uchumi na kuisababishia hasara Serikali ya jumla ya Euro milioni 2.
|
|
WAANDISHI WAKIWA WAMEMZONGA MAHALU BAADA YA HUKUMU |
|
MAHALAU AKITOKA HUKU AKIWA AMEONGOZANA NA MAWAKILI WAKE |
|
Balozi Profesa Mahalu
akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushinda kesi yake katika
mahakama ya kisutu leo.
|
|
akili wa Balozi Profesa
Mahalu Bw. Alex Mgongolwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
mteja wake kushinda kesili iliyokuwa ikimkabili kwenye mahakama ya Kisutu
jijini Dar es salaam.
|
|
Balozi Profesa Mahalu
katikati akitoka nje ya mahaka ya Kisutu huku akiwa ameongozana na mdogo wake
Mirasi Rama kulia ni Wakili wa kujitegemea Mabere Nyaucho Marando.
|
|
Aliyekuwa
Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu (kulia), akikumbatiana
kwa furaha na mmoja wa ndugu zake baada ya kushinda kesi yake katika Mahakama
ya Kisutu, Dar es Salaam leo, wakati wa kutolewa hukumu wa kesi yake ya
kuhujumu uchumi na kusababishia hasara Serikali ya Euro milioni 2 wakati akiwa
balozi nchini humo. Profesa Mahalu ameshinda katika hukumu iliyotolewa na
Mahakama hiyo
|
|
PROFFESA COSTA MAHALU |
No comments:
Post a Comment