BM BARBERSHOP KINONDONI

Sunday, August 19, 2012

DADA WA KIMANYEMA ASHA BARAKA AENDA KWAO KIGOMA KUJIPANGA

ASHA BARAKA-THE IRON LADY



Mkurugenzi wa ASET Mama Asha Baraka (The Iron Lady) amewasili Kijijini kwao KUNDUKA kilichopo Wilaya Mpya ya UVINZA iliyokuwa Wilaya ya Kigoma Vijijini miaka miwili iliyopita. Akiongea na Mwanatanga kwa simu muda mchache baada ya kuwasili Kigoma Asha Baraka amesema amekuwa na kawaida ya kufika Kijijini kwao kila inapofikia wakati wa EID kwa ajili ya kuwarehemu Ndugu zake waliotangulia mbele ya Haki akiwepo Baba yake Marehemu Ramadhani Baraka.

Mwanatanga pia ilipata fursa ya kuongea na Kiongozi wa Ukoo wa kina Baraka Mzee Ally Baraka na kutanabahisha kuwa Mwanae huyo Asha Baraka amefika Jana Usiku na sasa wako pamoja baada ya kutoka Msikitini. "Binti tuko naye hapa tumetoka msikitini muda si mwingi, nasasa tunajiandaa kufanya mazungumzo naye ili ATUJUZE mwenendo wa biashara zake huko Darisalamu hususan Bendi yake ya Twanga Pepeta ambayo nasi inatufanya tupate Mkate wetu wa kila siku. Marehemu kaka yangu Ramadhani wakati wa uhai wake alikuwa na tabia ya kutukusanya wakati kama huu na kufanya DUA ya pamoja ya kuwakumbuka wana BARAKA waliotangulia mbele ya Haki. Miongoni ma masuala ambayo huwa yanajusishwa ni pamoja na kuzulu Makaburi ya Wapendwa wao na kumuomba Mungu awaepushe na Moto pia kuomba Mungu kuhusiana na Kazi zao za kila siku ziwekewe Baraka kama lilivyo jina la Ukoo wao.

Aidha wakati dada mtu akiwa Kijijini kaka yao Mkubwa Baraka Msiilwa amepata balaa baada ya kuvamiwa na Majambazi Juzi usiku eneo la Salender  Karibu na Ubalozi wa Urusi. Tukio hilo lilitokea wakati Baraka Msiilwa akiwa natoka Msikitini Jirani na nyumbani kwake Upanga (Tarawei) majira ya saa nne na nusu usiku. Baraka Msiilwa aliimabia Mwanatanga kuwa tukio hilo lilitokea baada ya kupata Pancha hivyo aliamua kuapaki gari pembeni ili afungue tairi kwa ajili ya kubadilisha. Ghafla alitokea mtu na kuanza kumtaka ampatie fedha. Baraka alitanabahisha kuwa kwakuwa alikuwa kwenye vazi la Kanzu ambalo halikuwa na Mfuko aliwaambia watu hao ambao walizi kuongezeka na kufikia Kumi na kitu hivi kuwa hakuwa na pesa. Baada ya kuona hivyo walianza kuvunja vioo vya gari lake aina ya Lexas rangi ya Kijani na kuiharibu ikiwa ni pamoja na kuchukua Site Mirrors na vitu vingine ambavyo wezi hao walidhani vinaweza kuwasaidia kupata pesa wakienda kuviuza. 
MZEE KALALA NA ASHA BARAKA
Wasamalia wema waliokuwa ni walinzi jirani na eneo hilo walikimbilia kituo cha Polisi Salaender na polisi walifika mara moja na wezi hao kutokomea kwenye Pori la Salender. Jitihada za Polisi zimewezesha kupatikana kwa baadhi ya vitu ikiwemo baadhi ya vitambulisho muhimu pamoja na ATM Cards za Bwana Baraka. Aidha Baraka alipata majeraha kufuatia pirukushani hiyo iliyompelekea kushindwa kusafiri kwenda Kigoma KUHIJI kama ilivyo Desturi yao.

Asha Baraka anarajia kurejea baada ya Iddi na kuahidi kuja na nguvu mpya itakayowashangaza wengi. Alitia msisitizo kuwa WAPINZANI WAKE WAKAE CHONJO KWANI AMECHOKA KUHUJUMIWA. Alisema "Najua maadui zangu wamezoea kunionea na kunifanyia hujuma kwenye biashara zangu. Nimekuja kuomba ushauri kwa familia yangu kama nilivyofanya kipindi cha MCHINGA SOUND na Mungu alisikia DUA yangu. Ninaamini hata safari hii atanisikia na kuniaelewa na mwisho wa siku atanionyesha njia. Najua Mungu niwetu sote mimi pamoja na maadui zangu lakini najua Mungu humpa anachostahili yule anyemfitini mwenzake kwa HUSDA.... Ishaalha Mungu atanilipia punde" alimalizia.

Aidha mwanatanga alimdodosa zaidi mama Asha kwa kumuuliza maswali mawili ya KIZUSHI.
1. Dada Asha umeenda huko kurenew HIRIZI??? maana wapinzani wako wamekuwa wakilalamika kuwa wanafanyiwa mambo ya Kishirikina japo hawajawahi kukutaja wewe lakini kwakuwa wewe ni mpinzani wao kama wanavyodai hebu tuweke wazi.

JIBU: Kaka Deo mimi siishi kwa kutegemea Mizizi ila naishi kwa imani za Kumtegemea Mungu kama Muislam Mcha Mungu. Dhana ya Ushirikina huwezi kuiweka mbele kama wewe si muumini wake. Hivyo nadhani hao wanaozusha hayo basi huenda wanafanya hayo. Huku kwetu Kigoma tunajulikana kuwa wakali wa Masuala hayo hivyo pindi tunapokuja kusalimia ndugu zetu basi dhana kama hizo hujengwa, je tusije kuwasalimia ndugu zetu?? Kama kuna imani hizo za mimi kuja huku kufanya ushirikina basi tungoje tuone hatima ya hiki nilichokuja kufanya. Ila NITARUDI KIVINGINE KABISA NAKUAPIA.
ASHA BARAKA NA SWAHIBA WAKE MAMAA SAKINA (WOTE NI WENYEJI WA KIGOMA)
Swali la Pili-Mbona mdogo wako Omary Baraka hajaenda Kigoma???
Unajua baada ya Kaka Baraka kupata matatizo ya kuvamiwa na Majambazi ilibidi aahirishe ili amsaidie kaka kwenye kuwatafuta wahusika pamoja na matibabu ya Kaka Baraka kwakuwa Mke wake yuko UK, lakini wote ilikuwa tuje KUHIJI.

Mwisho alisema - EID MUBARAK KAKA DEO!!!!!!

No comments:

Post a Comment