Familia za wachimba migodi
waliouliwa na polisi wa Afrika Kusini, wakati wa mgomo wa Alhamisi, zimekuwa
zikipita mahospitali kuwatafuta jamaa zao. Wake wa wachimba migodi wanasema
polisi na mameneja wa kampuni ya mgodi hawakuwapa orodha ya wachimba migodi 34
waliouwawa na wengine wengi waliojeruhiwa kwenye mapambano hayo.
Polisi wanasema sasa
wanashirikiana na mameneja wa mgodi kutoa orodha kuu, lakini haiwezi kufichua
majina ya wachimba migodi zaidi ya 200 waliokamatwa. Rais Jacob Zuma ametangaza
kuwa ataunda tume ya kuchunguza mauaji hayo. Rais wa chama cha wafanyakzi
kisichokuwa rasmi, ameiambia BBC kwamba wanataka tume ya kimataifa na iliyo
huru.
No comments:
Post a Comment