|
MOJA KATI YA MABANGO YALIYOTUMIWA NA EXTRA BONGO HUKO UGHAIBUNI
|
Bendi mahili ya Extra Bongo chini ya Uongozi wa Kamarade Ally Choky Mzee wa Picha ya Ndege imerejea leo kutoka kwenye Ziara Nchi za Scandinavia iliyowachukua wiki kadhaa. Akiongea na Mwanatanga Ally Choky alisema "Kwakweli ziara yetu imekuwa ya mafanikio makubwa sana ambayo pia imetutengeneza Soko Kimataifa. Ziara hii imekuja kutokana na umahili wa Mcheza shoo Nguli aliyehamia Bendi hiyo akitokea Twanga Pepeta Comrade Super Nyamwela.
|
HOSEA BASS AKIFANYA MAKAMUZI |
Nyamwela alitanabahisha kuwa miongo kadhaa iliyopita alikutana na wazungu hao kwa nyakati tofauti na kuwafundisha jinsi ya kucheza shoo za Kiafrika ambazo huwa zinapendwa sana na Wazungu. Kupitia uelewano huo wazungu hao walifanya mawasiliano na Super Nyamwela na kumtaka aende na kundi la watu kumi na nne na yeye mwenyewe kwa ajili ya kufanya maonyesho ya miziki ya Kiafrika. Hakuwa na hiana Nyamwela aliona ni vyema kuongozana na Bendi yake ya Extra Bongo ambayo imekuwa ya Mafanikio Makubwa sana kwake binafsi na Bendi yake. Meneja wa Bendi hiyo MUJIBU ameiambia Mwanatanga kuwa Extra Bongo itakuwa kwenye Mapumziko kwa wiki Mbili na baadaye itaendelea na Maonyesho yake kama kawaida ili kuwaonyesha kile kilichofanywa na Bendi hiyo huko Ughaibuni.
|
SUPER NYAMWELA AKIWAFUNDISHA WAZUNGU KUCHEZA SHOO UGHAIBUNI |
Pamoja na hilo pia Meneja huyo amewaasa washabiki na Wapenzi wa Muziki wa Dansi kupenda vyao kwakuwa yeye ameshakuwa kwenye Bendi za Kikongo na sasa za Kitanzania ila akashangazwa na tabia iliyojitokeza ya Kuchukuliana wanamuziki kwa Kigezo cha Maslahi kwa kuasa kuwa Umakini inabidi uchukuliwe na Wanamuziki wenyewe kwani yawezekana kabisa wakawa wanajichimbia Kaburi kwenye Tasnia hiyo ya Muziki wa Dansi.
|
KAMALADE ALLY CHOKY, BOB KISSA NA ATHANAS |
Aidha mwanatanga iliongea na Mcheza Shoo Danger Boy ambaye alitanabahisha kuwa yeye hakuwa mgeni sana kwenye Nchi hizo kwakuwa ameshawahi kwenda mara kadhaa na Bendi ya Twanga Pepeta ila ametanabahisha kuwa amejifunza kitu kipya na wapenzi wake wajitokeze pindi maonyesho yao yatakapoanza kwakuwa anavitu vipya vya kutoka Ughaibuni.
|
OTILIA AKIONGOZA MASHAMBULIZI STAJINI |
Mwanatanga haikuishia hapo iliongea na baadhi ya Wacheza shoo akiwepo mwanadada Mahili aliyetokea Bendi ya Twanga Pepeta Otilia ambaye naye haukuwa na maelezo tofauti nayale ya Danger Boy. Wanamuziki wengine walioongozana na Bendi hiyo ni pamoja na; Martin Kibosho, Hosea Bass, Rama Pentagon,Athanas na wengine wengi.
|
SUPER NYAMWELA |
|
DANGER BOY |
No comments:
Post a Comment