BM BARBERSHOP KINONDONI

Monday, August 20, 2012

GAZETI LA NYAKATI TUOMBENI RADHI WAKATOLIKI


Nikiri kuwa sifahamu wamiliki wa gazeti hili la Nyakati. Lakini ni ajabu linajiita gazeti la kikristo!. Ingawa nilikuwa nimejizuia kuandika kuhusu ujinga na Mtazamo wa watanzania wengi juu ya dhana ya FREEMASON, lakini naona ni muhimu kutia neno juu ya toleo hili linalojiita la kikristo. Kwa kweli binafsi najisikia aibu kama Mkristo kuhusishwa na udaku na upuuzi kama huu wa kutoa juu habari yenye kuashiria kiongozi Mkuu wa wakristo duniani (mchungaji wa universal church) Papa Benedicto wa 16 kuwa ni freemason.

Jaribio hili naamini (Imani hii ni baada ya kutafiti kwa kina) ni mwendelezo wa kejeli ya VIJIDHEHEBU UCHWARA vya kikristo vyenye kupinga kanisa Katoliki. Nimechagua sana maneno hapa hivyo yeyote asianze kusema nimetukana au kukashifu imani ya mtu. Papa Benedicto akiwa halifa wa mtume Petro na amethibitisha pasipokuacha shaka kuwa mlinzi wa imani ya kristo, sasa huu uhuni wa kujaribu kumwita freemason unatoka wapi kama siyo kwa watu wenye matatizo makubwa ya uelewa wa mambo?

Katika uwezo wangu NALAANI kitendo hiki cha gazeti hili na kuliomba liache upuuzi wa namna hii leo na hata baadaye. Kanisa katoliki siyo kichaka cha kuficha wezi na wajanja ambao wakitafuta namna ya kuganga njaa zao wameamua kuacha kweli na kujianzishia VIJIDHEHEBU huku wakijipachika vyeo kama Mitume na Manabii na wala  Kanisa Katoliki popote duniani haliwezi lenyewe ama taasisi zake au mkatoliki yeyote mwenye akili za chini kuruhusu na au kuchaoisha UGORO kama huu ulio kwenye gazeti hili leo.

Jana hapahapa kwenye blog ya mjengwa gazeti la KISIWA limekosolewa kwa kutoa habari yenye picha za kutengeneza na kuifanya ya kiimani leo tena tunashuhudia matusi ya wazi kwa Kiongozi aliyeheshimika Karne nyingi tangu wamiliki na babu wa wamiliki wa gazeti hili uchwara hawajazaliwa. Gazet Nyakati liwaombe radhi Wakatoliki.

Mkatoliki aliyekasirika sana;
Ludovick
0715 927100
Nakuunga Mkono Bwana Ludovick…
Mimi Deo Mutta Mwanatanga nimezaliwa kwenye Ukatoliki na Nitafia kwenye Ukatoriki haiwezekani Udhalilishaji huu ukavumiliwa nalaaani mara sabini Gazeti hili.

No comments:

Post a Comment