Shirikisho la |Soka Tanzania (TFF) limepokea Hati ya
Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa wachezaji 11 wa nje kati ya 14 walioombea usajili
na klabu mbalimbali za Ligi Kuu.
Wachezaji walioombewa usajili Yanga na tayari ITC zao
zimepatikana ni Nizar Khalfan kutoka Vancouver Whitecaps ya Canada, Didier
Kavumbagu (Atletico Olympic- Burundi) na Mbuyu Twite kutoka FC Lupopo ya
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Kwa upande wa Simba ni Musa Mude (Sofapaka, Kenya) na Daniel
Akuffor (Stella Abidjan, Ivory Coast) wakati Mtibwa Sugar ni Shabani Kisiga
timu ya El Itihad ya Oman.
Waliopata ITC kwa upande wa Kagera Sugar ni Wilfred Ojodale Ame
na Benjamin Efe Ofuyah wote kutoka FC Abuja ya Nigeria. Wengine ni Deangelis
Silva kutoka New Road ya Nepal kwenda Coastal Union, George Odhiambo kutoka
Randers FC ya Denmark kwenda Mtibwa Sugar na Jerry Santo kutoka Tusker, Kenya
kwenda Coastal Union.
Wachezaji ambao wameombewa usajili na ITC zao bado
hazijapatikana ni Salum Kinje na Pascal Ochieng wa AFC Leopards, Kenya kwenda
Simba na Ayoub Hassan Isiko kutoka Bull FC, Uganda kwenda Mtibwa Sugar.
Bado klabu ambazo hazijakamilisha usajili na kupata ITC zina
fursa ya kufanya hivyo hadi Septemba 4 mwaka huu ambapo dirisha litafungwa.
Pia TFF imetoa ITC kwa wachezaji wanane walioombewa kwenda
kucheza mpira wa miguu katika nchi za Kenya na Msumbiji kutoka katika klabu
mbalimbali za hapa nchini.
Wachezaji hao na klabu wanazokwenda katika mabano ni
Abdallah Ally Abdallah (CD Madchegde, Msumbiji), Almasi Khatib Mkinda
(Ferroviario da Beira, Msumbiji), David Naftali (Bandari, Kenya) na Hassan
Hassan Mustafa (CD Madchegde, Msumbiji).
Wengine ni Meshack Abel (Bandari, Mombasa), Mohamed Banka
(Bandari, Kenya), Thobias Davis Silas (CD Madchegde, Msumbiji) na Thomas
Maurice (Bandari, Kenya).
No comments:
Post a Comment