Alphonce
Modest, anavyoonekana kwa sasa.
|
Nimesoma habari kupitia gazeti la
Championi kuhusu hali mbaya ya kiafya ya mchezaji mkongwe aliyewahi kuchezea
Simba kwa mafanikio makubwa na pia kucheza Taifa Stars kwa kipindi kirefu sana
tena kwa kiwango cha juu Alphonce Modest.
Mchezaji huyu kwa mujibu wa Gazeti la Championi
anasumbuliwa na figo na alikuwa amelazwa Bugando Mwanza na hali yake kimaisha
ni mbaya kumudu matibabu. Alphonce Modest amewataja Juma Kaseja na Mrisho Ngassa
kama wachezaji pekee wanaomsaidia. Namkumbuka mchezaji huyu alivyokuwa na nidhamu kubwa,mpole na mtu wa dini na
hasa soka lake akiwa moja ya beki namba tatu bora kuwahi kutokea Tanzania.
Hali ya soka huko nyuma kifedha ilikuwa mbaya zaidi ya sasa na wachezaji wengi wamebaki maskini.
Hali ya soka huko nyuma kifedha ilikuwa mbaya zaidi ya sasa na wachezaji wengi wamebaki maskini.
Naomba nitoe wito kwa TFF ifanye juhudi za kumsaidia Alphonce Modest ikibidi uwekwe utaratibu wananchi tumsaidie kuchangia tulicho nacho ili Modest ajue tunathamini mchango wake ktk Taifa hili na iwe motisha kwa vijana tunaowahimiza washiriki michezo.
Pole sana
Alphonce Modest,Mungu mwenye huruma akupe nafuu ya haraka ili uendelee kujenga
Taifa letu. Kampouni ya Msama Promotion imekuwa ya Kwanza kuchangia Matibabu ya
Mchezaji huyu kwa kutoa Jumla ya shilingi milioni moja kupitia Mratibu wa Tamasha
la Injili la Pasaka Tanzania, Alex Msama Mwitta. TFF pamoja na Simba Sports
Club oneni aibu na tambueni mchango wa Modest kwa kumsaidia kupata matibabu.
Said Kilumanga Mtanngazaji wa Channel Ten pamoja na Saleh Ali ndiyo
wahamasishajiwakubwa wa zoezi hili la uchangishaji wa matibabu ya Modest. Mungu
mpe afya na apone kwa haraka. Alex Msama akielezea jinsi alivyoguswa hadi akaamua kumsaidia Modest na
kutoa mwito kwa Watanzania kumuunga mkono kwa kumsaidia mchezaji huyo wa zamani
ambaye anahitaji fedha za kumtibia katika taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili
(MOI)
Modest anasumbuliwa na
ugonjwa huo tangu mwaka 2011. Kwa yeyote aliyeguswa na tatizo lake awasiliane
na Mtangazaji wa Channel Ten, Said Kilumanga (wa pili kulia) kwa kupitia simu
namba 0718 427426 au Mhariri Kiongozi wa Champion, Saleh Ally.
Alphonce
Modest akitoa shukrani kwa Msama na kuelezea jinsi ugonjwa huo ulivyompata na
kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, jijini Mwanza kwa
mwaka mzima wa 2011.
|
Said
Kilumanga ambaye ni mmoja wa wahamasishaji, waliowezesha kupatikana msaada huo
kutoka kwa Msama, akiendelea kuhamasisha umma kumsaidia kwa hali na mali Modest
apate kupona.
|
Saleh Ali ambaye pia ni mmoja wa wahamasishaji, akiwaomba wasamaria wema kuendelea kumsaidia Modesti kwa hali na mali |
Alphonce
Modest akitembea kwa taabu huku akisaidiwa na mdogo wake Francis.
|
Tumchangieni Alphonce Modest jamani huu ndio ubinadamu.Tulimshangilia enzi zake akiwa na timu ya taifa sasa anaumwa sio kumwachia Kaseja na Ngassa kwa uzuri wa roho zao jukumu lote. TFF wacordinate na wao kutoa msaada. Halafu TFF waweke sera ya kuwasaidia wote waliowahi kuchezea Taifa. Sio mchezaji anakua hoi bin taaban halafa wao wanakula ganzi.
ReplyDelete