BM BARBERSHOP KINONDONI

Friday, August 24, 2012

FULL STORY YA TWO O'CLOCK KIGALI LEO HII HAPA



Timu ya dar es Salaam Young Africans  Mabingwa mfululizo wa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, wameanza vema kwenye ziara yao Nchini Rwanda baada ya kuifunga timu ya Rayon Sport mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Amahoro mjini Kigali.Mabao ya Yanga yalifungwa na Hamisi Kiiza “Diego” kwenye dakika ya pili na baada ye mshambuliaji KINDA Simon Msuva kutupia la pili dakika 12. Kikosi cha Yanga kilikuwa hivi kwenye mechi ya leo:
1. Ally Mustafa ‘Barthez’, 2.      Shadrack Nsajigwa “Babu” /Stefano Mwasyika, 3.      Oscar Joshua/Mbuyu Twite, 4.      Nadir Haroub ‘Cannavaro’,5.      Kevin Yondan,6.      Athumani Iddi ‘Chuji’/Frank Damayo,7.      Simon Msuva,8.      Haruna Niyonzima/Omega Seme,9.      Didier Kavumbangu,10.   Hamisi Kiiza/Jerry Tegete na11.    Nizar Khalfan/Shamte Ally. 
 
Timu ya Yanga ilicheza mpira wa kufundishwa uliotawaliwa na pasi zenye macho wakati wote na kuwazidi wapinzani wao kwa kiwango kikubwa sana. Yanga ilikuwa ina uwezo wa kufunga mabao zaidi kama washambuliaji wake wangetumia vema nafasi zote walizotengeneza. Yanga itashuka tena dimbani kumenyana na Polisi siku ya Jumapili na kwa mujibu wa ratiba ya awali, wanatakiwa kurejea Dar es Salaam Jumatatu.
Awali, Yanga ilikuwa icheze pia na mabingwa wengine wa zamani wa Kombe la Kagame, APR, lakini kutokana na timu hiyo kukabiliwa na mgogoro hivi sasa uliosababisha kufukuzwa kwa kocha Mholanzi, Ernest Brandy na nafasi yake kupewa kocha mzalendo kwa muda, imeshindwa kuchezwa.
Mchezaji Said Bahanuzi hakuambatana na timu ya Yanga kutokana na matatizo ya kifamilia. Msafara wa Yanga una jumla ya watu 42 ikikwa ni pamoja na wachezaji 28, Maofisa 5 wa benchi la Ufundi na viongozi wanane




VIONGOZI 
Mwenyekiti Yussuf Manji,  Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga.      Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini Mama Fatma Karume, Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini Francis Kifukwe na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini Seif Ahmed ‘Magari’ Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Abdallah Bin-Kleb.      Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Salum Rupia.
 
BENCHI LA UFUNDI 
Kocha mkuu - Tom Saintfiet, Kocha Msaidizi - Fred Felix Minziro,  Kocha wa makipa- Mfaume Athumani, Meneja Hafidh Saleh, Daktari, Sufiani Juma, Mtunza vifaa Mahmoud Omary ‘Mpogolo’,  
WACHEZAJI 
Wachezaji ni makipa: Yaw Berko, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Said Mohamed. 
Mabeki Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Juma Abdul, Oscar Joshua, Stefano Mwasyika, David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondan, Ibrahim Job, Ladisalus Mbogo na Mbuyu Twite; 
Viungo Athumani Iddi ‘Chuji’, Juma Seif ‘Kijiko’, Salum Telela, Simon Msuva, Shamte Ally, Omega Seme, Idrisa Rashid, Nizar Khalfan, Haruna Niyonzima, Frank Domayo, Rashid Gumbo, Nurdin Bakari na  Washambuliaji; Hamis Kiiza ‘Diego’, Jerry Tegete na Didier Kavumbangu.

No comments:

Post a Comment