IMANI MADEGA MWANASHERIA |
ALEX MGONGOLWA MWANASHERIA |
LYOID NCHUNGA MWANASHERIA |
MABINGWA
wa Ligi Kuu Bara, Simba ya jijini Dar es Salaam imewasilisha barua Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF), wakimpinga Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria, Maadili na
Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho hilo, Wakili Alex Mgongolwa, pamoja na wajumbe
wake wawili kwa madai ya kutokuwa na imani nao.
Wajumbe
waliopingwa sambamba na Mgongolwa ni waliowahi kuwa wenyeviti wa klabu ya
Yanga, mawakili Lloyd Nchunga na Iman Mahugila Madega. Pingamizi hilo la Simba,
linatokana na kutokuwa na imani na viongozi hao katika kuamua suala la usajili
wa wachezaji waliozua utata, Kelvin Yondani na Mbuyu Twite, ambao awali Simba
inadai iliwasajili kabla ya Yanga kuingilia kati na kuwanyakua.
Kamati
hiyo ilikuwa ikutane jana na leo kwa ajili ya kupitia usajili wa klabu za Ligi
Kuu Bara na Ligi Daraja la Kwanza, lakini kutokana na kusogezwa mbele kwa ligi
hiyo, wanatarajiwa kukutana katika tarehe itakayopangwa baadaye. Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga ‘Mr.
Liverpool’ alisema wamewasilisha barua hiyo ili kuomba kushughulikiwa kwa ombi
lao kwa hofu ya kutotendewa haki.
Kamawaga
alisema kuwa Mgongolwa pamoja na kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo, pia amepata
kuwa mjumbe wa kamati za Yanga, huku Madega na Nchunga nao wakiwa ni wanachama
waadilifu na waaminifu wa klabu hiyo, hivyo ni rahisi kuipendelea. Aliongeza
kuwa kutokana na wajumbe hao wa kamati kuwa na damu ya Yanga, wanaamini
hawatatoa maamuzi sahihi kuhusiana na suala linalohusu utata wa usajili wa
wachezaji hao, hivyo TFF haina budi kutumia busara kuwaondoa.
Hivi
karibuni, Mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail Aden Rage, alitangaza kujiuzulu
ujumbe wa kamati hiyo, kabla ya Rais wa TFF, Leodegar Tenga, kukutana naye na
kumweka sawa, hivyo kubadili msimamo wake.
Kamati
ya katiba ,sheria na hadhi ya wachezaji inaongozwa na mwenyekiti Alex
Mgongolwa, makamu mwenyekiti Husein Mwamba na wajumbe Imani Madega,Venance
Mwamoto,Omari Gumbo ,Ismail Aden Rage na Lloyd Nchunga. Suala la kujiuliza ni
je vipi kuhusu Aden Rage na Omari Gumbo ambao nao ni wanachama wa Simba?Kwasasa
Rage ndio Mwenyekiti na Omari Gumbo kabla ya Uongozi wa sasa alikuwa makamu
mwenyekiti wa klabu hiyo.
Kumbe ndio maana Simba wanapokwa haki zao; kesi ya mwana kondoo kumpelekea chui. Halafu wanachekelea Simba kupokwa wachezaji wao kumbe ni umafia mtupu.
ReplyDelete