BM BARBERSHOP KINONDONI

Wednesday, August 29, 2012

POLISI WAACHA LINDO NYUMBANI KWA MKUU WEA MKOA NA WIZI KUFANYIKA

Jeshi la polisi Mkoa wa Njombe linawashikilia askari wawili waliokuwa lindo nyumbani kwa mkuu wa mkoa baada ya kutokea wizi usiku wa kuamkia siku ya sensa ambapo watu wasiofahamika waliingia nyumbani hapo na kuiba kompyuta mpakato moja, simu 3 mbili zikiwa nia aina ya Nokia ambazo ni mali ya watoto wa mkuu huyo wa mkoa.

Kamanda wa polisi kamishna msaidizi wa Polisi Bw.Fulgence Ngonyani amesema, tukio hilo lilitokea wakati nyumbani hapo wakiwepo walinzi ambao ni askari Polisi namba G15414 PC Ombeni na G 5455 PC Mohamed wanahojiwa kuhusiana na tukio hilo.

Kutokana na tukio hilo mkuu wa mkoa alisema kumekuwepo uzembe kwa askari Polisi wanaokuwepo Lindoni hapo kwani mara nyingi wamekuwa wakiacha lindo na kwenda kusikojulikana na kurudi wakiwa wamelewa, na kwamba kuna wakati wamekuwa wakitumia uda mwingi kulala na kuacha lindo.

Akizungumzia suala hilo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Aseri Msangi ametoa duku duku lake ama kero kuhusu askari hao kwamba tabia hiyo ya askari ameiona kwa muda mrefu na hiyo siyo mara yao ya kwanza kuondoka na kuacha lindo.

Amesema kuwa kuna siku alimkuta askari akiwa amelala ndani ya moja ya magari kati ya yaliyopo nyumbani hapo na kumwamsha akiwa fofo.

No comments:

Post a Comment