BAADA YA UKIMYA WA MUDA MREFU
HATIMAYE KALALA JUNIOR AAMUA KUFUNGUKA HIZI NI JUHUDI BINAFSI KATI MWANATANGA NA DADA YAKE KALALA JUNIOR BI. MARIA EMMANUEL KALALA.
NAMNUKUU KALALA " Kaka Deo Mutta nakuheshimu
sana mimi nimeamua kupumzika Muziki kidogo ili nijipange kwa ajili ya Shule na
Biashara, Ninasikia tetesi nyingi sana mara Ninaenda Twanga
Pepeta, Mara ninaenda Mashujaa Musica mara Extra
Bongo yote nayasikia. Mimi nimeamua
kupumzika na kusimamia Jengo langu kule BOKO ambalo sasa linaelekea Ukingoni.
Pili nimeamua kufanya biashara kufuatia Mafao yangu baada ya Mgao kutoka Band
ya Mapacha
Watatu ambako nilikuwa ni Hisa pale kama Mkurugenzi. wiki hii
nasafiri naenda China na Dubai kwa ajili ya Maandalizi ya Kibiashara.
Unayoyasikia mtaani hayana ukweli wowote na wala sina mpango wa kufanya Muziki
kwasasa zaidi ya kutoa Albam yangu Binafsi itakayowashirikisha baadhi ya
Wasanii Nguli wa Muziki wa Kizazi Kipya na Dansi. Muziki ninaupenda ninaweza
nikarejea kama mambo yangu ya kibiashara yatakapokuwa yametengemaa. Anayetaka
kujua habari zaidi anitafute Mwenyewe Kalala
Junior na sikueneza habari zisizo na Ukweli wowote. Kinywa changu
ndiyo Msemaji wangu. Natarajia kupata Mshauri wa kimaisha na Punde nitamtangaza
Hadharani na huyu atanisimamia kwenye kila Jambo.. iwe kimziki au kibiashara.;
Naomba Washabiki wangu wajue hivi nawewe kaka yangu tambua hivi pia. Wakati
ukifika nitawajulisha wadau na Mashabiki wangu kwenye Media Zote kuhusu HATIMA
yangu Kimziki. Mbona rafiki yangu wa Karibu MRISHO NGASSA kaamua kwenda Simba
BADALA YA YANGA??? hata miye si ajabu kuwa Mfanyabiashara. Nikirejea kwenye
Muziki kila mtu atajua na nitakuja kivingine kabisa." MWISHO WA KUNUKUU.
No comments:
Post a Comment