BM BARBERSHOP KINONDONI

Monday, August 6, 2012

TWANGA PEPETA YASALIMU AMRI YA WAISLAMU

Gazeti la KIU linalomilikiwa na KIU INVESTMENT CO. LTD na kupigwa chapa na Imprint kwenye toleo lake no. ISSN: 0856-7948 Na.1083 la Agosti 3-5, 2012 lilitoa habari iliyokuwa na kichwa cha Habari kilichosema BANGO LA TWANGA PEPETA KUUTAJA MWEZI MTUKUFU MASHIKH TISA WATOA TAMKO. Toleo la Gazeti lilihanikiza na kupambwa na Picha ya Mufti Mkuu wa Waislamu Shaaban Bin Simba, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhajji Mussa Salim, Mkurugenzi wa African Stars Mama Asha Baraka, Mmiliki wa Bendi ya Akudo Impact Alhaji na Mheshimiwa Mbunge Juma Athumani Kapuya pamoja na Mkurugenzi wa Band ya Mashujaa Musica Mama Sakina kuwa wamekuwa wakiendelea kufanya maonyesho ya Miziki ya Dansi kwenye Kumbi mbalimbali wakati wa Mwezi huu MTUKUFU wa RAMADHANI.

Aidha Gazeti la KIU lilitoa maelezo kuwa Mama Asha Baraka amepewa Siku tano kutoa Mabango au abadili dini, wakati Band ya Akudo Impact ilimtupia Mpira Alhaji Kapuya wakati Mama Sakina ameitibua famiklia yake. Baada ya taarifa hizi mwanatanga ilijaribu kuvinjari kwenye maeneo ya kumbi ambazo bendi hizi huwa zinafanya maonyesho yake na kurudi na taarifa hii;
Mkurugenzi wa ASET Mama Asha Baraka
African Stars Band Twanga Pepeta-Mkurugenzi wa Band ya Twanga Pepeta alikutana na Mwanatanga saa chache baada ya kusoma taarifa hizi kwenye Gazeti la KIU nayeye alikuja na Kauli hii. "Mimi nilikuwa China nimerejea leo kwa shughuli zangu za kibiashara, mimi kama Muislamu huwa bendi yangu haifanyi maonyesho wakati wa Mwezi wa Ramadhani, Jumamosi iliyopita Baada ya kombe la Kagame uongozi wa ASET ulifuatwa na baadhi ya wadau wakati mimi niko China na kuomba kupatiwa Burudani kufuatia ushindi wa Yanga. Bango lililowekwa pale mango Garden liliwekwa kwa misingi hiyo kwa mujibu wa taarifa nilizopatiwa na Viongozi wa Band pamoja na Mmiliki wa Mango Garden. Baada ya kupata taarifa hizo niliwaamulu mara moja kutoa bango hilo na mabango yote ambayo yanaihusu bendi ya Twanga Pepeta yakiwemo yale yazamani ili KUTII AMRI HALALI YA MASHEIKH WANGU ambayo waliitoa kupitia Gazeti la KIU. Sisi kama wamiliki wa Bendi tunatii na kuheshimu DINI yetu ya KIISLAMU na huwa hatuna utamaduni wa kufanya maonyesho wakati wa Mfungo wa Ramadhani kwani niwakati wetu Waislamu kushiriki SUNA hii ya FUNGA kwa Imani yetu." Mwisho wa Kunukuu. Mwanatanga ilipita eneo la Mango Garden na kukuta hakuna Bango hata moja la Twanga Pepeta Zaidi ya kuona Bango la Band ya Mashauzi na AKUDO, hivyo ilidhirisha wazi kuwa ASET wametii amri halali ya Mashekh ndani ya Dakika Chache baada ya kuona Habari hii chini ya usimamizi wake mwenyewe Mama Asha Baraka. 

Mheshimiwa Kapuya hakupatika kueleza juu ya Sakata hili juhudi zinaendelea ili kuona kama anaweza kutoa maelezo kama alivyotii AMRI Mkurugenzi wa Twanga Pepeta Bi. Asha Baraka.
MHESHIMIWA ALHAJI ATHUMAN JUMA KAPUYA
 Aidha Mwanatanga ilijaribu kumtafuta mama Sakina ili atoe tamko juu ya Jambo hili imeshindikana. Kwakuwa Mwanatanga ni mtu wa karibu na Mejeja wa Mashujaa Musica Ndugu. Martin Sospeter alimtafuta kwa simu na alidai kuwa hana taarifa hiyo kwakuwa yuko na Bendi kwenye ziara ya Mikoa ya nyanda za Juu Kusini Ruvuma na Mbeya.
BENNY KINYAIYA, ASHA BARAKA NA MAMA SAKINA WA MASHUJAA MUSICA

2 comments:

  1. Hili jambo sio jema, hakuna haja ya viongozi wowote wa dini kushinikiza watu kuacha kufanya kazi zao za halali kisheria kwa kuwa eti ni mwezi wa ramadhani. Mtu awachwe kuamua kwa hiyari yake sio kushinikiza. Je kama hakuna kipato hao wanamuziki watakula mawe? Kwanza wengi sio waislamu, kwa nini kuwatesa. Kufunga ni jambo la kiroho, hivyo anayefunga atafuata maelekezo ya dini kwa hiyari na sio kuwanyima watu wengine uhuru wao.

    ReplyDelete
  2. Hivi mtu analazimishwa kufunga au kuheshimu dini? Nisaidieni jamani. Nadhani imani ni ya mtu mwenyewe. Anyway, kwa kuwa tupo pamoja lazima watuheshimu tumalize kufunga ndio waendelee na dansi lao... Hongera Twanga Pepeta kwa "KUTII AMRI...."

    ReplyDelete