WAKATI
taarifa za kurejea nchini kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven
Ulimboka zinasemwa bila wausika kuthibitisha viongozi wa Jumuiya hiyo na Umoja
wa Madaktari Tanzania (MAT), wanatarajia kukutana Jumanne Augosti 7, 2012
kujadili tukio zima lililomkumba kiongozi huyo. Baada ya kikao hicho, madaktari
hao watakutana na familia yake na kisha kumuuliza Dk Ulimboka kama angependa
kilichomtokea kiwekwe wazi kwa jamii.
Dk
Ulimboka ambaye alikuwa anaratibu mgomo wa madaktari uliokuwa ukiendelea nchi
nzima, alitekwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Jumatato ya Juni 27
mwaka huu na kupelekwa katika msitu wa Pande, nje kidogo ya Jiji a Dar es
Salaam, ambako aliteswa na kujeruhiwa vibaya. Katika tukio hilo daktari huyo
aling’olewa meno mawili na kucha za mkono mmoja na baadaye kulazwa katika
Kitengo cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalum (ICU) katika Taasisi ya
Mifupa (MOI).
Baada
ya hali yake kuzidi kuwa mbaya Juni 30 mwaka huu, alisafirishwa kwenda Afrika
ya Kusini kwa ajili ya vipimo na matibabu. Kusafirishwa kwake kulifuatia
taarifa ya jopo la madaktari lililokuwa linamhudumia kutoa taarifa kwa
madaktari bingwa kuhusu mabadiliko ya afya yake. Taarifa za kurejea kwa Dk
Ulimboka zimezagaa katika mitaa mbalimbali jijini Dar es Salaam, huku baadhi ya
watu wakizijadili katika mitandao ya kijamii.
Katibu
wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Edwin Chitage, alisema kati ya Agosti 7 au
8, 2012 viongozi mbalimbali wa MAT na Jumuiya ya Madaktari, watakutana kujadili
suala la kiongozi huyo. “Ndani ya siku mbili hizi (Agosti 7 au 8) viongozi
tutakutana na kujadili ripoti ya matibabu ya Dk Ulimboka na tutajadili kama
tuvieleze vyombo vya habari ama laa,” alisema Dk Chitange.
Hata
hivyo Dk Chitange alisema hatua hiyo itategemea na kauli ya familia ya Dk
Ulimboka na yeye mwenyewe (Dk ULimboka) kwa kuwa na wao pia watashirikishwa.
“Dk
Ulimboka na familia yake tutawashirikisha katika mambo ambayo tutayajadili,”
alisema Dk Chitage. Alipoulizwa kama kiongozi huyo wa madaktari sasa anaweza
kufanya shughuli zake kama awali, alisema hana uhakika kwa kuwa hana taarifa za
ndani zaidi .
No comments:
Post a Comment