BM BARBERSHOP KINONDONI

Thursday, August 23, 2012

KALALA JUNIOR BACK HOME.... THE RETURN OF VANDAMME

 Akiongea kwa KUJIAMINI kuonyesha kuwa amekua na amerejea nyumbani baada ya kutoka na kwenda kutafuta Mwanamuziki Kalala Hamza Kalala leo milango ya saa 04:52 Ukumbi wa Mango Garden Mbele ya waandishi wa habari alitamka maneno machache yafuatayo Nanukuu “Mimi Kalala Hamza Kalala AKA Kalala Junior niliondoka Twanga Pepeta takriban mwaka mmoja na nusu uliopita baada ya kuunda Bendi ya Mapacha Wanne ikiwajumuisha wanamuziki Wanne Kalala Junior, Charles Baba, Jose Mara na Khalid Chokoraa. Baada ya kuunda kundi hili Charles Baba aliamaua kuendelea kubaki na Twanga Pepeta hivyo jina likabadilika na kuwa Mapacha Watatu (Kalala Junior, Khalid Chokoraa na Jose Mara). Tulifanya kazi pamoja kama ndugu na Wapiganaji wa Ukweli ili kufikia Malengo ambayo tulikuwa tunayatarajia. Miezi kadhaa iliyopita niliwaaga wenzangu kuwa NARUDI NYUMBANI lakini hawakuamini hivyo leo natamka rasmi kuwa KWA RIDHAA YANGU MWENYEWE NIMEAMUA KUREJEA NYUMBANI TWANGA PEPETA. Kalala alimalizia kwa Usemi wa “Koti likikubana livue” nami leo koti nimeona limenibana nimeamua kurejea nyumbani “Twanga Pepeta SUGU Kisima cha Burudani”. Mwisho wa kunukuu.
Baada ya maelezo hayo Kiongozi wa Bendi ya Twanga Pepeta Saleh Iddi Kupaza “SACCOSS” alisema ndugu waandishi kwa niaba ya Wanamuziki wa Twanga Pepeta tunamkaribisha kwa moyo MKUNJUFU Kalala Junior baada ya kurejea nyumbani. Hapa ni kazi tu na ninajua kuwa hilo unalijua na nina imani tutafanya vizuri zaidi kwakuwa najua uwezo wako Karibu sana Mdogo wangu.
Baada ya Maneno hayo ya Kupaza Waandishi walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali kama Ifuatavyo:

SWALI LA KWANZA: Kalala Junior ulipoondoka kwenda Mapacha ulisema unaenda kutafuta chako je kwanini leo umeamua kurejea Twanga Pepeta Je kipi kimekushinda huko ulikokuwa???
JIBU LA KALALA: Nilikwenda kutafuta na nilichokitaka nimekipata sasa narudi nyumbani ila zingatia usemi wangu kuwa Koti likikubana Livue…. Kichekooooo hahahahahahaah.

SWALI LA PILI : Je umekuja na lipi jipya ndani ya twanga pepeta??
JIBU LA KALALA: Nimekuja na mengi ikiwepo staili mpya ya Uchezaji, Utawala wenye NIDHAMU ambao hata ukienda Mapacha hili la NIDHAMU nililisimamia kwa HAKI nawala halina Ubishi. Katika kudhihirisha hili la Tungo tayari nimeshatunga nyimbo iitwayo NYUMBANI NI NYUMBANI. Ndani ya wimbo huo nimewashirikisha wafuatao:
Kwenye Drum amepiga mdogo wangu James Kibosho, tumba amepiga Kaposhooo, gitaa la Kati – George Kanuni, Solo Kapiga – Sele Mumba na Kinanda Victor Nkambi Mwanasumnbawanga. Kwenye uimbaji nimeshirikiana na Kaka yangu Salehe Kupaza Master Filling, Badi Bakule Jogoo la Mjini, Uncle Venna, Janeth Isinika, Ibrahim Kongoro (Mirinda Nyeusi) na mimi mwenyewe.

Rap nipo mimi mwenyewe, Mirinda Nyeusi, J4 na Greyson Semsekwa.
Hapo imepigwa shoo ya kufa mtu nataka kuwadhihirishia Wadau wangu kuwa mimi ni Mwanamuzi na (MUSICIAN) wa Karne nyingine kabisa waniache.

Baada ya Maneno haya Kalala junior aliimba Chouras ya Wimbo huo mpya wa NYUMBANI NI NYUMBANI akishirikiana na Salehe Kupaza nanukuu Kipande hicho: “Mengi yalisemwa sana na mabaya kunipakazia, Na mengi yatasemwa sana lakini hayataweza, Narudu Nyumbani leo Twanga Pepeta SUGU, Hapa Yuko Baba Hapa Yuko mama Narudi nyumbani leooooooooo.
Baada ya hapo Kalala alikamata Drum kuonyesha Uwezo wake na baadaye Gitaa la Bass. Alimalizia kwa Usemi huu.
VANDAME IS BACK TAKE CARE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

 














 












 


 





 














No comments:

Post a Comment