Baada ya kuwa kimya kwa muda Mrefu Mwanamuziki aliyekuwa kwenye kundi la Mapacha 3 Kalala Hamza Kalala Almaarufu Kalala Junior kesho atatambulisha Single yake aliyoiita NYUMBANI NI NYUMBANI na USHIRIKA NI SAWA NA KOTI LIKIKUBANA LIVUE. Mwanamuziki huyu Nguli anatarajia kuwa na Bendi yake Mwenyewe baada ya kushindwa kuendelea na USHIRIKA. Kalala ametanabahisha kuwa ni vema sasa akatoa msimamo wake na amesema tayari ameshatunga Nyimbo mbili KALI atakazozitambulisha kesho atakapoongea na Waandishi wa Habari.
No comments:
Post a Comment