Zikiwa
zimesalia wiki mbili kabla ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kuanza
chini ya usimamizi wa chombo huru yaani kampuni, kuna kila dalili ya
ligi hiyo kusogezwa mbele kutokana na ukweli kuwa mambo kadhaa bado
hayajafikiwa ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa chombo kitakacho simamia
ligi hiyo.
Kwa mujibu wa maelezo ya Rais wa
shirikisho la soka hapa nchini Leordiga Chila Tenga wakati wa ufunguzi
wa mkutano mkuu wa TFF mwezi April mwaka huu alisema ligi ya mwaka huu
itaendeshwa na chombo kingine tofauti na kamati ya ligi ya TFF ambacho bado hakijaundwa.
Mwenyekiti wa
kamati ya ligi ya ligi ya TFF Wallece Karia amesema kamati yake bado
inaendelea kusimamia mambo kadhaa ya kuanza kwa ligi hiyo licha ya Kamati ya Utendaji
ya TFF iliyokutana wiki mbili zilizopita tayari kuidhinisha ligi hiyo
kusimamiwa na vilabu vyenyewe, lakini bado structure kamili ya uongozi
wa vilabu haijajipanga sawasawa kusimamia ligi hiyo msimu huu.
Wallace amesema kimsingi kamati yake ya
ligi itakuwa inakoma kufanya kazi ya kusimamia ligi hiyo baada ya
uzinduzi wa chombo hicho ambacho bado hakijaeleweka.
Rais wa TFF Leordigar Tenga anatarajiwa kuzindua chombo hicho mapema
kabla ya ligi kuanza huku mambo kadhaa ikiwemo muda wa kufungwa kwa
dirisha la usajili na kusikilizwa kwa mapingamizi haujafikia mwisho.
Yapo mambo kadhaa ambayo yanapaswa
kukamilishwa kabla ya ligi hiyo kuanza ambapo kwasasa ndiyo kwanza TFF na kamati ya ligi ya sasa kwa kushirikiana na viongozi wa vilabu wako
katika mazungumzo na madhamni wa ligi hiyo kampuni ya simu za mikononi
ya Vodacom.
Mambo mengine ni mtihani wa waamuzi yaani Copa test, pamoja na
uthibitisho wa viwanja gani vitatumiwa na vilabu shiriki katika ligi
hiyo mambo ambayo unaweza kuona kama ni madogo lakini yanahitaji muda na
mazungumzo na makubaliano baina ya pande zote husika.
Wallece Karia amesema bado kamati yake
inaendelea na mchakato wa kuelekea kuanza kwa ligi hiyo kwa kushirikiana
na secretarieti ya TFF pamoja na viongozi wa vilabu ili kukamilisha
taratibu zote muhimu za kuanza kwa ligi hiyo ikiwemo suala la mdhamini
Vodacom ambaye muda wa mkataba wa sasa wa Vodacom kuelekea kufikia
ukingoni August 31.
MSIKILIZE WALLACE KARIA
MSIKILIZE WALLACE KARIA
Mwezi April Rais Tenga mbele ya wajumbe
wa mkutano mkuu wa TFF alisema lazima katika msimu wa ligi wa 2012/2013
ligi hiyo itakuwa ikisimamiwa na chombo huru ambacho kitakuwa na
majukumu ya kuendesha na kusimamia ligi ikiwa ni pamoja na suala la
ratiba na kusimamaia adhabu.
Suala lingine ni usimamiaji wa mapato
pamoja na kutengeneza management kwa kuajiri watendaji wakuu na kuajiri
mhasibu wao jambo ambalo mpaka sasa hakuna dalili za watendaji hao kuwa
tayari wameshaandaliwa.
No comments:
Post a Comment