BM BARBERSHOP KINONDONI

Wednesday, August 15, 2012

OKWI KWENDA AZAM NI HADAA TUPU, MILIONI 15 ZILIZOTOLEWA NA SIMBA KWENDA AZAM KWA AJILI YA KUMALIZA SAKATA LA REDONDO LIMEDHIHIRISHA UHALISIA

Lile sakata la Usajili wa Mchezaji Ramadhani Chombo Redondo juu ya Kuvaa Uzi MWEKUNDU pale Msimbazi limefikia ukomo wake baada ya Simba kufanya kikao kati yake na Azam na kufikia Muafaka wa kuilipa Azam Jumla ya shilingi milioni kumi na tano za Kitanzania na kumaliza kabisa tatizo lililokuwa limejitokeza.

Wachunguzi wa masuala ya kisiasa wameita kiini macho kwakuwa Azam iliapa kutomruhusu mchezaji Redondo kuvaa Uzi mwekundu kwakuwa ni mali yao na ana Mkataba halali wa kuendelea kuchezea timu hiyo ya CHAMAZI. Hali hii imeweka bayana kuwa Simba na Azam niwatoto wa Baba mmoja hivyo wale waliokuwa wakidhani kuwa itafikia kipindi Simba na Azam wakwaruzane juu ya hili WAMEULA WA CHUYA. Mifano ya Uswahiba ipo likiwemo suala la Mchezaji Mrisho Ngassa, Jeba na Wengine wengi ambao wamekuwa wakipisha kwenda Simba na Azam.

Suala linalopamba vyombo vingi vya habari sasa hivi kwamba Okwi anaenda AZAM kwa gharama yoyote ile ni uzushi na halitawezekana. Habari hii ni aina nyingine ya kutengeneza PR kati ya Azam na Simba kuficha ukweli kuwa hawa ni Maswahiba. Time will tell!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment