JENGO
la Ofisi ya Mamlaka ya Mji mdogo Mombo wilayani Korogwe limeteketa kwa
moto usiku wa kuamkia jana na kusababisha hasara, ikiwa ni pamoja na
kuungua nyaraka mbalimbali pamoja na samani.Akizungumza
na waandishi wa habari, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo,
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa lilitokea majira ya
saa 8:00 usiku.Alisema kuwa, moto huo ulisababisha baadhi ya ofisi zilizopo ndani ya jengo hilo kuungua.
Gambo
alizitaja ofisi hizo kuwa ni Ofisi ya Mhasibu, Masijala na Ardhi na
cheti cha Usajili wa Mamlaka ya ofisi za mji mdogo huo huku kumbukumbu
zote za ofisi hizo zikipotea.Alisema,
serikali imeunda kikosi kazi kitakachoshirikiana na vyombo vya ulinzi
na usalama wilayani humo kuchunguza chanzo cha tukio hilo. Gambo alisema watakaobainika kuwa chanzo cha moto huo ulioisababishia hasara serikali, watachukuliwa hatua za kisheria.
Mkuu
huyo alisema wanaangalia uwezekano wa kuwa na sehemu maalumu
zitakazotumika kuhifadhia nyaraka muhimu za kiserikali ili inapotokea
majanga kama hayo, kuwepo na kumbukumbu.Alisema Jeshi la Polisi kwa sasa linawashikilia walinzi wa jengo hilo kwa uchunguzi zaidi.Naye,
Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji huo, Richard Rwezile, alisikitishwa na
tukio hilo huku akitupa lawama kwa gari la zimamoto ambalo lilishindwa
kufika katika eneo hilo kwa wakati, hatua iliyochangia moto huo kusambaa
kw
No comments:
Post a Comment