BM BARBERSHOP KINONDONI

Wednesday, August 29, 2012

WATANZANIA 251 WAMEPOTEZA MAISHA KWA AJALI ZA BODABODA JIJINI DAR ES SALAAM NDANI YA MIEZI MITATU


Jumla ya watu 251 wamepoteza Maisha kwa ajali zilizohusisha usafiri wa Bodaboda jijini Dar es salaam katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita jijini. Katika ajali hizo zaidi ya watu 1,289 wamepata majeraha huku wengine wakipata ulemavu wa kudumu. Wadau wa Usalama barabarani wameainisha kuwa, biashara holela kwa madereva wasio na mafunzo ni chanzo mama cha ongezeko la ajali kwenye vyombo hivyo vilivyoshika kasi kipindi cha hivi karibuni.

Baadhi ya waendesha bodaboda wamekana kuwa wao pekee ndiyo chanzo cha ajali bali ni kukosekana kwa umakini baina ya mamlaka za usalama pamoja na wamiliki wa vyombo vya usafiri. Kamanda poilisi kikosi cha usalama barabarani kamanda Mohammed Mpinga, ikiwa ni moja ya mbinu za kukabiliana na ajali kwa kushirikiana na wadau wa vyombo vya usafiri wamekutana jijini Dar es salaam na kuzindua mafunzo kwa madereva zaidi ya elfu moja yatakayotolewa bure kwa yeyote aliye na nia ya kuwa dereva bora wa bajaji na bodaboda jijini hapa.

Kwa upande mwingine Wizara ya Mambo ya Ndani bado ina kazi kubwa ya kufanya kwenye upenyo wa biashara huria na bado kuna mwanya wa uzembe katika kusimamia kiuhakika usalama wa vyombo vya usafiri, Nizar Jivani ni Rais wa chama cha wamiliki wa bodaboda na bajaji AAT.

Ajali za barabarani licha ya maangalizo mbalimbali yanayoatolewa zimeendelea kuwa wimbo wa kila uchao huku maisha ya wananchi yakiendelea kuteketea, na kubwa ikiwa ni ongezeko la kizazi tegemezi kutokana na wengi kuachwa wakiwa na ulemavu .

No comments:

Post a Comment