Omary Seseme - Mwanatamtam (African Revolution)
Mwaka 2006, wanamauziki kadhaa wa
zamani walijikusanya na kuanzisha bendi ambayo ilijulikana kama Tanza
Muzika. Bendi hii ilikuwa na wanamuziki kama akina Kasongo Mpinda
Clayton, Issa Nundu, Mukumbule Parashi na wengine wengi wazuri. Pamoja
na kuwa bendi nzuri walikosa vyombo na hivyo kuwa chini ya himaya ya
jamaa walioweza kuwa na vyombo ambao nao mwaka 2007 wakajitoa na hivyo
kundi hilo likavunjika.
Roy Mukuna na Rashid Mwezingo - Mwanatamtam African Revolutions
Baada ya kuvunjika kwa kundi hilo baadhi ya Wanamuziki walihamia Mwanza na kuungana
na kundi la Mwanza Carnival ambao ni pamoja na Roy Mukuna, Mukumbula Parashi, Issa Nundu, Bonny Chande na Omary Seseme. Miezi michache baadaye mfadhili wa kikundi akaanza kuugua na hivyo
kundi hilo kusambaratika tena. Wanamuziki wakaamua kurudi Dar Es Salaam
na kulikopelekea kujiunga kwa mkongwe mwingine ndugu Ally Yahaya, ambaye ni mpiga trumpet na kujipa jina jipya Super Kamanyola.
ANNA MWAOLE |
Benno Villa Anthony
Band ilipata mwaliko kwenye
bonanza la Villa Park Mwanza na baada ya hapo uongozi wa
Mwanza Villa Park ukaingia katika makubaliano ya kuifanya Super
Kamanyola kuwa resident Band. May 2010 bendi ikahamia rasmi Mwanza. Wanamuziki wanaounda kundi hili ni pamoja na;
1. Roy Mukuna, Saxophonist na Kiongozi wa Bendi,
2. Ally Yahaya Trumpetist na Katibu wa bendi,
3. Seseme Omary Solo
guitar na uimbaji,
4. Beno Villa Anthony mwimbaji na mpiga Keyboards na mshauri wa bendi,
5. Mukumbule Parashi muimbaji,
6. Rashid Mwezigo
mwimbaji,
7. Anna Mwaole muimbaji,
8. Bonny Chande Bass guitar,
9. John Hamisi
rhythm guitar, na
10. Duncan Matembe Drums.
Ally Yahaya na Roy Mukuna
Bendi hii inakumbusha mbali sana kwa kupiga miziki ya bendi mmbalimbali zikiwemo za Maquis,
OSS, Tancut Almasi, TP OK Jazz, African Fiesta n.k
No comments:
Post a Comment