MBUYU TWITE NDANI YA JEZI YA NJANO NA KIJANI KESHO DHIDI YA AFRICAN LYON
Klabu bingwa Afrika Mashariki na kati Dar Young Afrikans (Yanga )
kesho watashuka dimbani kucheza dhidhi ya timu Afrika Lyon mchezo wa kirafiki
utakao pigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mchezo huo
umeandaliwa na Kampuni ya VANNEDRIC(T)LTD kwa lengo la kutoa burudani kwa
wakazi wa jiji la Dar es salaam mara baada ya kumalizika kwa mwezi mtukufu wa
Ramadhani lakini pia ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya vikosi vya timu hizo
ambazo zinashiriki ligi kuu ya Tanzania bara.
Mchezo huo umepangwa kuanza saa 10 kamili na kila timu imeahidi kushusha
vikosi vyao kamili vilivyo sajiliwa msimu huu. Itakumbukukwa Yanga mara baada
ya kutwaa Kombe la Kagame bado haijashuka tena dimbani kucheza mchezo wowote
mbali ya kucheza mchezo mmoja na kombaini ya Kijitonyama. Hii itakuwa ni fursa
nzuri kwa mashabiki wa timu hiyo kongwe hapa nchini kuwaona kwa mara nyingine
tena wachezaji wao pamoja na mlinzi nyota aliyejiunga na Yanga msimu huu
akitokea APR ya Rwanda Mbuyu Twite.
Kwa upande wao African Lyon ambayo kwasasa inanolewa na kocha wa kigeni
raia wa Argentina Pablo Ignacio Velez inataka kutumia mchezo huo ili
kusahihisha makosa ya wachezaji wao baada ya mafundisho ya muda mfupi toka kwa
kocha huyo.
Viingilio ni katika mchezo huo ni Sh. 5,000/=, Sh. 7,000/=, Sh. 10,000/=
na Sh. 15,000/=.
No comments:
Post a Comment