BM BARBERSHOP KINONDONI

Tuesday, August 7, 2012

NAIBU WAZIRI WA AFRIKA MASHARIKI APATA AJALI MBAYA NA FAMILIA YAKE AKITOKEA BUNGENI KIBAHA




Wakati akifunga kikao cha Bunge cha jioni ya leo, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Anne Makinda aliwatangazia Wabunge kuwa Naibu Waziri wa Afrika Mashariki,  Mheshimiwa Abdallah Juma Abdallah Saddallah amepata ajali katika eneo la Tumbi, Kibaha Mkoani Pwani akiwa njiani kurejea Dar es Salaam, ndani ya gari hilo alikuwemo Dereva wake, Naibu Waziri, Watoto pamoja na Msaidizi wa shughulil za nyumbani. Spika alitoa taarifa kuwa majeruhi waliwahishwa hospitali ya Tumbi, Kibaha kwa matibabu zaidi.
 
Mwanatanga blog ilifuatilia taarifa hii kwakina na kubaini kuwa ajali hiyo mbaya ilitokea majira ya jioni wakati naibu waziri huyo akitokea Bungeni kuelekea jijini D'salaam akiwa na mkewe pamoja na watoto wake wawili, dereva wake ambaye aliumia vibaya na kukimbizwa hospital yaTumbi-Kibaha pamoja na mtumishi wa kazi wa nyumbani kwake. Aidha mashuhuda wa ajali hiyo akiwemno wamedai kuwa chanzo cha ajali hiyo inasemekana ni baada ya dereva wa Naibu Waziri kujaribu kulikwepa Lori alilokuwa akipishana nalo na hivyo gari lake kuhama njia na kupinduka.  .

Imeelezwa kuwa baada ya ajali hiyo umati wa wananchi wakiwemo vibaka walifika eneo hilo kutaka kupora mali mbali mbali ila hawakuweza kufanikiwa baada ya raia wema kusaidia kuepusha hali hiyo .Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinda alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo baada ya kuhojia na mwandishi wa habari hizi na kuwa hali ya naibu waziri huyo si mbaya sana zaidi ya dereva wake ambaye ameumia kichwani.". 

No comments:

Post a Comment