|
KALALA WA BANTU GROUP |
Mwanamuzi Kalala Hamza Kalala ameiambia Mwanatanga muda mfupi kabla ya Kupanda ndege kuelekea Mwanza na baadaye Urambo Tabora kwa ajili ya Mazishi ya Shemeji yako amesema kuwa mbali na Shughuli zake za kiabiashara anazifanya sasa hivi amekamilisha Single yake Ijulikanayo kwa Jina la Nyumbani ni Nyumbani. Ndani ya single hiyo Kalala amewashirikisha baadhi ya Wanamuziki wa Kizazi Kipya akiwepo Diamond Platnum, huku Rap ikihanikizwa na Rapa Ibrahim Kongoro almaarufu Mirinda Nyeusi. Single hiyo ambayo ina mistali ambayo inaonekana kana kwamba inaonya, kufundisha, kuasa, Kushauri na kuelekeza imetulia ikiwa na Midundo wa Dansi ambayo inachezeka.
|
KALALA ENZI ZA TWANGA PEPETA
|
Baadhi ya Vipande ambavyo vinasikika kwenye wimbo huo ni pamoja na KOTI LIKIKUSHINDA LIVUE, DOMO LA BABU LINANUKA UGORO LAKINI LIMEJAA HEKIMA, kipande ambacho Mwanatanga hakukielewa ni kile kinachosema RAFIKI SOKONI BORA KULIKO PESA MFUKONI. Mwanatanga ilimdadisi kwa kina juu ya semi hizi lakini Kalala alisema kuwa kaka DEO MUTTA mimi nizaidi ya Mwanamuziki hivyo nilikuwa najaribu kutoa Darasa kwa njia ya Sanaa ambalo najua pindi ikianza kusikika Redioni kila mmoja ataweka tafsiri zake lakini wimbo huu ni PART ONE hivyo utakuwa na muendelezo wake ambao utatoa ufafanuzi wa Wimbo huu wa NYUMBANI NI NYUMBANI" Mwiho wa kunukuu.
|
KALALA ENZI ZA MAPACHA |
Aidha Blog hii haikuishia hapo iliendelea kumdodosa ili kujua kama wimbo huu utatoka pekee au utakuwa kwenye Album??? Kalala Junior alisisitiza kwa kusema kuwa "Kaka unakumbuka Juzi tuliongea nikakuambia kuwa nimeamua kujishughulisha na Mambo yangu binafsi ikiwa ni pamoja na kufanya Biashara??? Lakini pia nilikuambia kuwa mimi Mziki uko kwenye Damu yangu hivyo siwezi kuacha Muziki na nikitaka kurejea kwenye Muziki NITAUAMBIA UMMA kwakuwa najua Mashabiki wangu wananimiss. Ngoja nijipange kwanza Kibiashara malengo yangu yakikamilika nitawaeleza watu ninachokusudia kufanya kwenye MUZIKI jambo ambalo najua limenijengea Heshima Nje na Ndani ya Tanzania. Nazidi kusema kuwa Namshukuru Baba na Mama Kalala, Waliokuwa Wakurugenzi Wenzangu pale Mapacha, Mama Asha Baraka, Mama Sakina, Nteze wa Nteze, Fredito Mopao, Mke wangu Mary Kalala, Rey Kigosi, Marehemu Steven Kanumba, JB, Wadau na Mashabiki na Wanamuziki wenzangu wooote kwani kila mmoja kwanafasi yake ana mchango mkubwa sana kwenye mafanikio yangu Kimuziki. Nikirejea Msibani kaka tutaongea kwa kina" Mwisho wa kunukuu.
|
KALALA WASASA MFANYABIASHARA
|
No comments:
Post a Comment