EMMANUEL OKWI KAZINI |
Mchezaji wa Simba SC EMMANUEL Okwi ambaye kwa siku kadhaa habari zake zilihanikiza kuwepo kwa sintofahamu juu ya Majaaliwa yake ya wapi atatokezea leo hii amewasili na kujiunga na timu yake ya Simba na leo amehudhuria Mazoezi ya Club yake ya Simba pale TTC Chang'ombe.
Mashabiki waliohudhuria mazoezi ya Simba walisikika wakisema KIKO WAPI wale Yanga Maneno tu hawana lolote haya sasa Okwi huyo hapo... Kule Ngassa huku Okwi shughuli imeisha.Awali iliripotiwa kuwa Mwanandinga huyu alikwenda Australia kufanya majaribio ya kucheza Soka huko na baadaye kurejea Uganda baada ya kushindwa vigezo vya kucheza Soka huko. Aidha habari ambazo zilitawala Mjini ni kuwepo kwa habari kuwa Kiongozi mmoja wa Yanga Bwana Abdallah Ahmad Bin Kleb alienda Kampala, Uganda kwa ajili ya kumshawishi ili achezee Simba na wakawa wamekubaliana kuwa alipwe mshahara wa dola za Kimarekani 3,000
Kufuatia kuwasili kwa Mchezaji huyu ni dhahiri sasa mjadala wa Emmanuel Okwi utakuwa umefungwa na ataendelea kutumikia Klabu yake ya Simba SC na Si Ulaya au si Yanga.
No comments:
Post a Comment