BAADHI YA WADADA WANAOUZA MIILI YAO - MACHANGUDOA |
Sifa
za Bwana zivume. natumai muwazima kumekuwa na changamoto katika kuhubili injili
ya kristo na kuhakikisha kuwa kila kiumbe anasikia hii habari njema ya Yesu
kristo. katika utafiti wangu mdogo nilioufanya niligundua kuwa
kuna makundi ambayo hayafikiwi kutokana na mazingira waliopo inakuwa ni
vigumu kuwahubiria, mara nyingi nimeona wainjilisti wakishuhudia na
kuhubiri katika vituo vya mabasi, masokoni, mahospitalini, nk vilevile mikutano
ya injili ambaye hapo mwanzo ilikuwa inaonekana inakusanya watu wengi imepoteza
uwezo huo kwa sasa hasa katika jiji la Dar es salaam na inatakiwa itafutwe
njia mbadala. lakini kuna makundi ambayo kwa njia moja au nyingine ni vigumu
kwao kuweza kufika kwenye mikutano hiyo ya injili, mfano watoto wa mitaani,
wavuta unga na machangudoa, machangudoa huwa wanabadilisha ratiba zao mchana
wana lala na usiku wao wanakuwa macho kiasi kwamba wao kufika kwenye mikutano
ni ndoto kwenda na ukisikia changudoa kaokoka basi ujue ni nguvu ya Mungu tu, hivyo
inatakiwa hatua za makusudi kukutana na kundi hili. ziko changamoto nyingi
katika juu ya wokovu jamii ya machangudoa.
MACHANGUDOA ENEO LA SINZA |
- Unatakiwa uwafuate kwenye viwanja vyao na wanaotakiwa kuongea nao kwa nyakati hizo za usiku ni Wanaume. Kama akienda mwanamke mwenzao huwa wanaona kuwa wanadhihakiwa (unawajoki) na wala hawatakusikiliza. Mwanaume wanaweza kumsikiliza na kujibu maswali yake maana wanajua mwisho wa yote watapata chochote.
- Kabla changudoa hajaokoka anatakiwa ajue ataishije baada ya kuokoka maana walio wengi wanaishi kwa kutegemea kazi hiyo tu. Kwa misingi hivyo lazima kuwe na fungu litakalomfanya mtu huyo kuweza kuyafanya maisha yaendelee kinyume na hapo atarudi mtaani kuuza mwili wake ili apate chochote.
- Mazingira wanayoishi Machangudoa ni kwenye kwenye Magheto hivyo inabidi pia atafutiwe mahali pa kuishi kinyume na hapo wenzake watamrejesha Ghetto na hatimaye kurejea kule ulikomtoa.
Vilevile
kuna mambo mengine zaidi yanayosababisha watu hawa kufanya biashara hii ya
kuuza miili yao ikiwa ni pamoja na: Ugumu
wa Maisha – Ila kama mtu ukiokoka utajua tu kuwa biashara hii ni utumwa ambao
shetani anawatumikisha wengi kwa kuwatia pepo wa ngono kwa imani hizi za Ugumu
wa Maisha.
Mbali na Imani hizi zote ukweli ni
kwamba kwa Yesu yote yanawezekana ila swali je nini nani atakaye waendea MACHANGUDOA
na kuwaandalia mazingira mazuri ya kumfanya mtu huyo aache kazi hiyo.
Changamoto hapa ni suala la Ajira Mbadala kwakuwa yakubidi umtafutie kazi
mbadala. Pili mazingira mbadala na uangalizi wa karibu ambao utamfanya ajisikie
vizuri katika maisha yake mapya na kupata mafundisho na maombi na kumfanya
aachane kabisa na marafiki zake wa zamani alio wazoea.
MADADA POA ENEO LA SINZA AMBIANCE |
Wakati wa utafiti tulibahatika kuonana
na mama mmoja ambaye yeye kwa sasa ni mama Askofu wa Kanisa la TAG ambaye alisema
kuwa alifanikiwa kuwashuhudia machangudoa na kuwafanya waokoke na kuachana na
kazi ya uchangudoa, maelezo yake yalikuwa hivi. “Baada ya kugundua kuwa alikuwa
anaishi na machangudoa mtaa mmoja alianza kufanya maombi ya kuwaombea na
kufanya urafiki nao na kuzoeana nao baada ya hapo ilibidi awe anaongea nao
mmoja mmoja anasema kuna siku alimchua changudoa na kumwingiza chumbani kwa
mume wake na kuanza kumwambia habari za Yesu tena kwa kuanza
kumwonyesha heshima kubwa aliyopewa ya kuingizwa chumbani kwa mume wake na wao
machangudoa walikuwa wamemzoea huyo mama na walikuwa wakimwita mama. Baada ya
mazungumzo na yule changudoa alikubali kuokoka na kuachana na kazi ya
uchangudoa na mungu hana hiana akaanza kumpa marupurupu ya wokovu dada huyo
akafanikiwa sana na kupata nafasi ya kwenda Marekani na hadi sasa yuko huko kwenye
huduma ya Benny Hinn.
Kwahiyo iko changamoto ya kuwafikia
watu hawa ambao wainjilisti wengi wametuwa hawamudu kufikia kundi hili kwa kuwa
wengi wamefungwa na nguvu za giza na wamekata tamaa ya maisha na kuona
bora wafanye biashara hiyo haramu ambayo ina madhala makubwa sana kiroho
kimwini na hata kisaikolojia. kama wewe si mwinjilisti basi chukua nafasi hata
ya kuwaombea ili Mungu akutane nao na Mungu ainue watu watakaokuwa na
mzigo kuwafikia watu hao.
BARIKIWA.
Mathayo 6:33 Utafuteni kwanza ufalme
wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa.
No comments:
Post a Comment