BM BARBERSHOP KINONDONI

Sunday, August 19, 2012

NO WAR-ASEMA JK .... RAIS WA MALAWI JOYCE BANDA APUMUA


Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Jakaya Mrisho Kikwete amekanusha habari kuwa Tanzania inajiandaa kuingia vitani kupigana na Nchi ya Malawi kugombania Ziwa Nyasa au Ziwa Malawi kama linavyotambulika nchini Malawi ambako kwasasa kuna Kampuni ya Kiingereza inayotafiti Mafuta kwenye ziwa hilo kwa niaba ya Nchi ya Malawi. 

Akiongea na Waandishi wa habari baada ya majadiliano kati yake na Rais wa Malawi Mama Joyce Banda huko Maputo, Msumbiji, Rais Jakaya Kikwete alisema “Tetesi za kuwepo kwa vita baina ya nchi hizi mbili yalikuwa yakitoka kwenye midomo ya ushawishi wa viongozi pinzani wa Kisiasa ili kujipatia umaarufu. Mimi ndiye Amiri Jeshi sijayaelekeza au kuyaagiza majeshi yangu kuingia vitani. Hivyo kama kauli hii haijatoka kwenye kinywa change basi taarifa hiyo siyo ya Kweli aslisema JK” "Namhakikishia dada yangu na watu wote wa Malawi kwamba hatuna nia wala mpango we kuingia vitani, hatuna matayarisho ya jeshi wala jeshi halijasogea popote kwani hakuna sababu" amesema na kuongeza kuwa “Mimi ndiye Kamanda Mkuu wa Majeshi na sijapanga wala kutoa maelekezo ya vita".

Kulikuwa na taarifa kutoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuwa majeshi ya Tanzania yamekuwa yakielekea kwenye mipaka ya Tanzania na Malawi pembezoni mwa ziwa Nyasa tayari kwa vita. Rais alisema nchi yangu imekuwa na uhusiano mzuri na nchi ya Malawi kwa miaka mingi sana na haina mpango tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
 

Rais amesema hayo, mbele ya Rais Banda na kuongeza kuwa Kumekuwa na sintofahamu ya muda mrefu kuhusu suala la mpaka na tayari maafisa wa pande zote mbili wameshaanza kulizungumzia Kwa nia ya kulitatua Kwa Amani."Tuviachie vyombo vyetu vifanye kazi, hebu tuvipe nafasi, wanasiasa na waandishi we habari wajiepushe na maneno haya yanayosababisha taharuki na chokochoko, hayana maana yeyote wwachie diplomasia ifanye kazi yake" Rais amesisitiza. Naye Rais Banda amesema amefurahishwa na kufarijika baada ya kuhakikishiwa kuwa hakuna vita na Rais Kikwete."Nimefarijika sana, suala hili limetusumbua sana, mpaka wa-Malawi wote wakaungana na kuwa kitu kimoja na kuzuia tofauti zao" amesema na kuvishukuru vyombo vya habari vya Malawi Kwa kuonyesha uzalendo na ukomavu katika suala hili. Rais Kikwete alikuwa Maputo, Msumbiji kuhudhuria kikao cha viongozi wa Jumuiya Ya Maendeleo Kusini Kwa Afrika (SADC) uliofunguliwa tarehe 17 August, 2021 na  umemalizika jana jioni (tarehe 18.august 2012).

Katika kikao Tanzania imechukua uenyekiti wa Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama kutoka Afrika ya Kusini ambapo uenyekiti wa SADC umechukuliwa na Msumbiji kutoka Angola, nafasi hizi ni za mwaka mmoja mmoja Kwa zamu.

Rais amesema hayo, mbele ya Rais Banda na kuongeza kuwa Kumekuwa na sintofahamu ya muda mrefu kuhusu suala la mpaka na tayari maafisa wa pande zote mbili wameshaanza kulizungumzia Kwa nia ya kulitatua Kwa Amani."Tuviachie vyombo vyetu vifanye kazi, hebu tuvipe nafasi, wanasiasa na waandishi we habari wajiepushe na maneno haya yanayosababisha taharuki na chokochoko, hayana maana yeyote wwachie diplomasia ifanye kazi yake" Rais amesisitiza. Naye Rais Banda amesema amefurahishwa na kufarijika baada ya kuhakikishiwa kuwa hakuna vita na Rais Kikwete."Nimefarijika sana, suala hili limetusumbua sana, mpaka wa-Malawi wote wakaungana na kuwa kitu kimoja na kuzuia tofauti zao" amesema na kuvishukuru vyombo vya habari vya Malawi Kwa kuonyesha uzalendo na ukomavu katika suala hili. Rais Kikwete alikuwa Maputo, Msumbiji kuhudhuria kikao cha viongozi wa Jumuiya Ya Maendeleo Kusini Kwa Afrika (SADC) uliofunguliwa tarehe 17 August, 2021 na  umemalizika jana jioni (tarehe 18.august 2012).

Katika kikao Tanzania imechukua uenyekiti wa Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama kutoka Afrika ya Kusini ambapo uenyekiti wa SADC umechukuliwa na Msumbiji kutoka Angola, nafasi hizi ni za mwaka mmoja mmoja Kwa zamu.

Banda alisema “Malawi inamiliki asilimia 100% ya Ziwa lakini Malawi itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kujadiliana juu ya jambo hili KIDIPLOMASIA zaidi kwakuwa vita haliwezi kuwa suluhisho muafaka kwenye kutatua tatizo hili.” Utata huu ulianza mwezi Julai 2012 kufuatia nchi ya Malawi kufanya utafiti wa Mafuta kwenye Ziwa hilo na Kampuni ya Surestream.

Wakati wa mkutano huo wa SADC uliofanyika nchini Msumbiji Rais wa Zambia Micheal Sata ndiye Mwenyekiti wa SADC kwasasa.  Rais wa Msumbiji Armando Guebuza aliwaomba washiriki kuwa mgogoro wa Mpaka kati ya Malawi na Tanzania kutoa mawazo na kuwashauri kutofikia kwenye hali ya vita. Aidha Rais Sata wa Zambia alitania kwa kusema kama Tanzania na Malawi wataanza Kupigana sisi tuko tayari kupokea wakimbizi.

 RAIS WA ZAMBIA MICHAEL CHILUFYA SATA

Msimamo wa Malawi kwenye Mgogoro huu ni kwamba ziwa Malawi ni mali yao tangu 1890 wakati wa Makubaliano ya Heligoland yaliyojulikana kama “HELIGOLAND TREATY” au “ANGLO-GERMAN TREATY” yaliyosainiwa kati ya Uingereza (United Kingdom of Great Britain, Ireland and German) kuhusu ugawanaji wa mali katika bara la Afrika.
Malawi pia wanasema Makubaliano ya Heligoland yalitiliwa nguvu tena mwaka 1963 kwenye makubaliano ya kuundwa kwa Umoja wa Nchi huru za Kiafrica (OAU) pamoja na makubaliano ya kuundwa kwa chombo kipya cha African Union (AU) mwaka 2002 na 2007 kwamba Wanachama wa Umoja huu wataheshimu mipaka iliyobainishwa wakati wa kupata UHURU.

Wake wa Marais wa Wakuu wa Nchi za kusini mwa Africa (SDC)  Katikati ni  Mke wa Rais wa Tanzania Mama Salma Kikwete  na wa kwanza kulia  ni mke wa Rais wa Zambia Dr. Christine Kaseba Sata  wakifuatilia majadiliano ya Mkutano huo mjini Maputo.
KUMBUKUMBU ZA WATANZANIA
Utotoni tuliimba wimbo huu wakati wa mchakamchaka uliojaa hisia za utaifa. Hii inamaana kuwa hata wakati ule utata huu ulikuwepo hivyo hili si jambo geni hata kidogo. Nakumbuka wakati huo Rais wa Malawi alikuwa Marehemu Dr. Kamuzu Banda (Wa Kumuyaya) yaani rais wa Maisha aliyekuwa Daktari wa Marikia Elizaberth wa Uingereza na baadaye kupewa zawadi ya kuwa Rais wa Maisha wan chi hiyo kwenye Koloni la Muingireza kama zawadi kufuatia kitendo ambacho inasadikiwa kilifanyika kwa Dr. Banda kutomuwezesha kupata motto (Castration) ili asiweze kuzulu Malkia wakati wa Matibabu.
DR. KAMUZU BANDA
Wimbo mwingine unaodhihirisha Mgogoro huu kuwa wa kitambo toka enzi za Mwalimu ni huu hapa: " Kipara cha Banda kina ukoko!"  Ni dhahili kuwa harufu ya Vita haikuanza Julai mwaka huu kama inavyotafsiriwa ila ni kutokana na Uungwana wa Watanzania tu.  Ukiingia ndani zaidi utagundua kuwa Tanzania na Malawi ni ndugu wa damu. Kuna hata simulizi za kweli za Watanzania upande wa pili wa Ziwa Nyasa waliokesha kusheherekea Uhuru wa Malawi, hivyo basi, tunaweza kabisa kumaliza mgogoro huu wa mpaka kidiplomasia kutamka, kuwa "Jambo la Malawi ni letu, shida yao ni yetu, Huzuni yao ni yetu na furaha yao ni yetu.
Tunashukuru kuwa Rais wetu Jakaya Mrisho Kikwete ni mwanadiplomasia. Mimi kama Deo Mutta Mwanatanga nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa JK anaweza kutuingiza katika Vita vya kiwendawazimu' dhidi ya  jirani na ndugu zetu wa Malawi (Wanyasa, Wangoni, Wapangwa, Wamatumbi, Wamwela, Wayao, Wandendeule na wengine wengi utawapata pande zote mbili za nchi hizi).
HAYATI MWALIMU JULIUS KAMABARAGE NYERERE RAIS WA KWANZA
UTANI KIDOGO:
Enzi za utoto ilikuwa hivi, kaka zetu walipotaka kufurahia wadogo zao tukipigana makonde,  walisubiri pale mmoja anapomkasirikia mwenzake. Haraka atatokea kaka na mchanga mkononi na kutamka kwa mmoja kati ya wawili walio kwenye magomvi na kusema “Haya, puta mchanga wangu  kama kweli wewe ni mwanamme!" Nani asiyetaka kuwa mwaname? Atauputa mchanga. Kisha kaka anamgeukia mwingine; " Haya sasa, nilipie ng'ombe wangu!". Kulipa ng'ombe ilikuwa na maana ya kuanza kurusha konde na hapo ugomvi ulianza rasmi!

Najua dhahiri kuwa miongoni mwetu kuna wenye kutamani vita, anayetamani vita ni mtu mjinga. Mwalimu alipata kutamka hivi " Vita si lelemama". Na katika dunia hii inasemwa kuwa chagua vita vyako kwakuwa vita vingine havina lazima ya kupiganwa.

Tofauti zetu na Malawi zinaweza kutatuliwa kwa mazungumzo ya kindugu kama Rais JK na dada yakeRais JB- Joyce Banda walivyotanabahisha.

Wakati huu hatuwahitaji tena kina kina Moses Nnauye kututungia nyimbo za Mchakamchaka, eti twende tukiimba; " Banda (Joyce) wa Malawi, Katuvalia Kitenge Cha Ngozi ya Mamba, Kututishia Watanzania,  Hatuwezi, Hatuwezi!".

WAKATI UMEBADILIKA HAKUNA ALIYE TAYARI KUPOTEZA AMANI TULIYOIGHARIMIA KWA MIONGO MINGI. NO VITA FULL STOP.


PICHA ZA MARAIS NA VIONGOZI MBALIMBALI WA KUKUMBUKWA KWENYE HISTORIA YA MGOGORO HUU.
RAIS WA KWANZA WA MALAWI DR. HASTINGS KAMUZU BANDA- WAKUMUYAYA
RAIS WA KWANZA WA TANZANIA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE



SIMBA WA VITA HAYATI RASHID MFAUME KAWAWA
MAREHEMU BRIGEDIA MOSES NNAUYE

RAIS WA AWAMU YA PILI MZEE ALLY HASSAN MWINYI

RAIS WA WAMU YA TATU MZEE BENJAMINI WILIAM MKAPA
RAIS BAKILI MULUZI WA AWAMU YA PILI MALAWI
RAIS WA AWAMU YA TATU MALAWI HAYATI BIGU WA MUTHARIKA

MWAMBAO WA ZIWA NYASA UPANDE WA TANZANIA























1 comment:

  1. Kaka uko deep! Safi sana kwa kutoa elimu hii kwa umma. watoto wengi hawayajui haya

    ReplyDelete