KOFFI OLOMIDE AKIONYESHA ISHARA YA NGUMI |
Mwanamuzi mashuhuri nchini kongo(DRC) Anton Akgeba Makila Mabe maarufu
pia kama Koffi Olomide aka Mopao Mokonzi, ameswekwa Lupango na kafikishwa kwa
Pilato kwa kosa la kumpiga mtayarishaji wake wa Muziki Diego Lubaki. Mwanamuziki
huyo alikamatwa na kufungiwa katika kituo cha Polisi na kufikishwa mahakamani
jumatano ya wiki hii.
Koffi alikamatwa kufuatia vurugu katika hoteli moja mjini Kinshasa. Waandishi wa habari
wanasema mahakama hiyo ya Kinishasa ilifurika kutokana na watu wengi kuja
kumuona kiongozi huyo wa bendi ya Quartier Latin akiwa kizimbani. Kesi hiyo iliahirishwa
hadi Alhamisi asubuhi wakati atakaposhitakiwa rasmi. Wakati wa kesi hiyo Koffi
Olomide aliwakilishwa na mawakili kumi (10).
Ugomvi kati ya mwanamuziki huyo na mtayarishi wake Bwana, Diego Lubaki ni juu ya pesa dola $3,680. Hakimu alimfahamisha mwanamuziki huyo ikiwa atapatikana na hatia ataenda jela miezi sita. Koffi Olomide ni gwiji wa muziki aina ya "soukous", mtindo uliotokana na jina la kifaransa "secouer", lenye maana ya kujitikisa au kujinengulisha na wachezaji wake vile vile wanatambulika kwa kunengua maungo.
No comments:
Post a Comment