HARAMIA WA SOMALIA MOHAMMAD SHIBIN AKISINDIKIZWA KWENDA JELA NA ASKALI BAADA YA HUKUMU |
Raia mmoja wa Somalia amehukumiwa
vifungo 12 vya maisha na Mahakama ya Marekani baada ya kumuona kuwa na hatia ya
kufanya makubaliano kwa niaba ya maharamia wa Kisomali kuhusu fidia ya kuachiwa
huru kwa mateka wa Marekani mwezi wa pili mwaka uliopita 2011.
Raia huyo wa Somalia Mohammad Shibin
(pichani juu ) amekutwa na makosa 15 yakiwemo ya uharamia na utekaji nyara. Kwa
mujibu wa mahakama hiyo Shibin alilipwa kati ya dola 30,000 na 50,000 kwa
kufanya makubaliano ya fidia juu ya mateka hao. Maharamia wa Kisomali
waliwateka raia wanne wa Marekani kwenye pwani ya Somalia na baadaye kuwauwa
pamoja na jitihada za jeshi la Marekani kutaka majadiliano kuhusu kuachiwa
kwao.
No comments:
Post a Comment