LEO NDUGU YANGU MAHMOUD RAMADHANI
ZUBERY WA BIN ZUBERY
www.bongostaz.blogspot.com
AMENIKOSHA SANA KAMALIZA MZIZI WA FITINA KITAALAM. UKIACHA UNAZI NA UKASOMA
HOJA ZAKE SITA KWA MAKINI UTAMUELEWA ILA UKIWA MNAZI MWENYE PUPA UTABAKIA
KULALAMA NA KUENDELEA KUONGOPEWA…FUATILIA HAPA CHINI NAMNUKUU.
MWANAHABARI MAKINI ... NA MTAFITI MAHMOUD RAMADHANI ZUBERY |
MASWALI SITA YA KUJIULIZA KUHUSU SIMBA
SC NA MAMBO YA LEO:
1.
Kwa
nini habari zilivuja Mwenyekiti wa Simba SC alimpa Mbuyu Twite dola za
Kimarekani 30,000, wakati sasa inaelezwa mchezaji huyo alipewa dola 10,000 tu
2.
Simba
ilisema ilimuongezea mkataba Kevin Yondan, je ilimpa na fedha? Na kama ilimpa
fedha mbona hazijavuja habari zozote juu ya fedha alizopewa, wakati inajulikana
hadi Felix Sunzu analipwa dola za Kimarekani 3,500 kwa mwezi?
3.
Simba
ilimsajili na kumpa fedha beki Lino Masombo kutoka DRC, tena inaelezwa ni fedha
nyingi tu, je baada ya kumtema bila kumpa muda wa kutosha kujiridhisha kuhusu
uwezo wake (mdogo au mkubwa), ili kukwepa kurudia makosa yaliyofanyika katika
kumtema Derrick Walullya, fedha hizo zinarudishwa au?
4.
Ukitazama
kikosi cha Simba kwa sasa utagundua wamesheheni viungo kibao, Amri Kiemba,
Jonas Mkude, Christopher Edward, Mussa Mudde, Haruna Moshi, Kanu Mbivayanga,
Mwinyi Kazimoto, Uhuru Suleiman, Kiggi Makassy, Salim Kinje, Ramadhan Singano ‘Messi’,
Mrisho Ngassa na Ramadhan Chombo ‘Redondo’, wakati mabeki wa kati ni Juma
Nyosso, Shomary Kapombe na Obadia Mungusa, (Zingatia, kiasili Kapombe na Maftah
kiasili ni viungo) je, hii iko sawa?
5.
Nani
huwa anashauri masuala ya usajili ndani ya Simba…Kusajiliwa au kukatwa kwa
mchezaji, je anafanya kazi yake vizuri?
6.
Kitaalamu
inafahamika kuwa kumchezesha mchezaji mechi kabla hajawa fiti kwa angalau zaidi
ya asilimia 50 ni kumtengenezea mazingira ya kuumia na tumeshuhudia majeruhi
wengi katika siku za karibuni Simba SC kwa leongo la kufurahisha mashabiki. Je
kwa nini Kocha Mkuu, Mserbia Milovan Cirkovick anaruhusu hali hii?
No comments:
Post a Comment