Malalamiko ya Simba leo kwamba mtoto
wa kigogo kaisadia Yanga kwenye Usajili wa Twite yananirejesha kwa Maprofesa wawili
Ndugu. Philemon Sarungi na Juma Athumani Kapuya wadau wakubwa wa Simba na
watumishi waliowahi kuwa kwenye Serikali kwa Miongo mingi na kuiumiza Yanga historia
inajirudia.
Maprofesa Philemon Sarungi na Juma
Athumani Kapuya walipokuwa wana ‘meno’ kwenye serikali ya Tanzania waliwasaidia
SANA Simba kuwaliza Yanga. Katika kuutambua msaada huo, kwenye Sherehe za Simba
Day, Simba walimpa tuzo Profesa Sarungi. Tuzo la jinsi hii lilishawahi kutolewa
kwa Professa Juma Athuman Kapuya miaka ya nyuma.
Proffessa Athumani Juma Kapuya
aliwaumiza Yanga mwaka 1999. Yanga wakiwa wamekwishatwaa ubingwa kwa matokeo ya
uwanjani kwa kuifunga Mtibwa Sugar mabao 2-1 katika mechi ya mwisho Uwanja wa
Uhuru (Shamba la Bibi) Dar es Salaam Professa Kapuya alitengua matokeo na kuipa
ubingwa Mtibwa iliyokuwa ya pili. LENGO
KUWAUMIZA YANGA KWA UNAZI WAKE.
Mwaka 2001 Professa Juma Athumani Kapuya
aliongeza timu katika Ligi Kuu kwa sababu zake mwenyewe bila kuzingatia Mkataba
wa udhamini wa ligi hiyo unasemaje, hali ambayo iliwafanya waliokuwa wadhamini,
Safari Lager wakajitoa na kuiponza Simba iliyokuwa bingwa kukosa zawadi.
Proffesa Juma Athuman Kapuya alishapangua
matokeo ya Ligi Kuu ili kuwabeba Simba na hata kubatilisha usajili wa
wachezaji, mfano Victor Costa ambaye mwaka 2005 alitakiwa kufungiwa kwa kusaini
Simba na Yanga lakini bwana mkubwa huyu akiwa Waziri wa Wizara ya Michezo na
Utamaduni alitumia Madaraka yake vibaya kwa kumidhinisha kuchezea Simba. AKINYA BATA KAHARISHA LAKINI KUKU AAH.
Ridhiwani ni mdau na Mpenzi wa Yanga
kama walivyo Sumaye, Kapuya, Ndugai, Zitto, Nasari, Sitta, Makala, Sarungi,
Ngeleja na wengine wengi NI HAKI YAKE YA KIMSINGI NA KIKATIBA.
No comments:
Post a Comment