Yanga inataka kuuhakikishia ulimwengu kuwa ipo kwa ajili ya kuendeleza soka na kuleta
mageuzi ya Mchezo wa Mpira wa Miguu hapa Tanzania. Awali nilitegemea kuwa timu
ya Azam itakuwa timu ya kwanza kuleta maendeleo baada ya kujenga uwanja wa
Kisasa kule Chamazi na kuajili makocha na wachezaji na kuwalipa Mshahara mkubwa
unaokidhi mahitaji ya Mwanamichezo angalau kwa kiasi Fulani kinachotumainisha.
Kinyume na hapo timu ya Azam ikabadilika na kuwa Tawi la Simba na sasa kuingia
kwenye Mgogoro baina yao.
Ukimya wa Yanga baada ya KUPOKWA
mchezaji Mrisho Khalfan Ngassa kwa mashirikiano ya Timu za Azam na Simba
ulinipa mashaka sana na kuona kuwa kumbe Yanga wamenywea. Niliposikia kuwa Mheshimiwa
Mbunge wa Tabora na Mwenyekiti wa Simba
SC alisafiri kwa takribani Kilomita 1,459.7 kwa Ndege ya Air Rwanda ili kupata
Sign ya Mchezaji Mbuyi Twite na kufanikiwa kumzidi ujanja Mjumbe aliyetumwa na
Yanga Abdallah Ahmad Bin Kleb.
Taarifa za Dhihaka zilitolewa
kupitia blog ya www.shaffihdauda.com kuwa Makamu Mwenyekiti wa Simba Bwana Geodfrey Nyange Kaburu
Pamoja na Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba SC Ndugu Zakaria Hans Pope wamemalizana
na kiungo mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa na wakati huo Mwenyekiti wa klabu ya
Simba SC Mheshimiwa Ismail Aden Rage (MB) amekamilisha utiliananji saini kati
yake na Beki Mahili Mbuyi Twite wa APR. Wachezaji wote hawa wawili Ngassa na
Twite walikuwa wanawaniawa pia na mahasimu wao ambao ni mabingwa wa Africa
Mashariki na Kati Yanga SC 2012/2013. Aidha blog hiyo ilionyesha ujumbe kutoka
kwa msemaji wa Simba SC Ndugu Ezekiel Kwamwaga kuwa “Kigali, saa nne kasoro asubuhi ya leo....Mbuyi Twite
anasaini mkataba wa kuitumikia Simba mbele ya Mhe; Ismail Aden Rage...Wakati
akipata kahawa, jamaa mmoja anaitwa Bin Kleb akapiga simu, "Twite, siye Yanga
tunakutaka sana tuambie tuje lini ili tumalizane....Akawekewa loud speaker;
akaambiwa Mzee, hapa napata cappuccino nikiwa na Mwenyekiti wa Simba...Kleb
akakata simu....2-0....1-0 ilikuwa Ngassa.......Jamani Simba ina watu
kibao....Jamani Simba...Mi Casa Es Su Casa”
Ujumbe wa aina hiyo kutoka kwa Luis
Sendeu uliandika hivi “Batu ba Yanga bamekuja na mipesa mingi so nimesign nao wako
byee hawa wa Simba hawajatomboka byee iko na maneno mingi mipesa hakuna!”
Jana nikapata habari ambazo zilinimaliza
nguvu na kunichanganya kuwa; Simba ilimsainisha kweli beki Mbuyi Twite wa APR.
Utiaji saini huo kweli ulifanywa na Mwenyekiti Mheshimiwa Alhaj Ismail Aden
Rage, kwa dola za Kimarekani, 10,000, na si 30,000 kama ilivyoripotiwa. Yanga walikasirishwa
na KIBURI na maneno ya Kebehi kutoka kwa Simba hivyo walikaa kimya na kujipanga
kwa kuwa VITA NI VITA. Yanga iliamua kupanda Dau kwa Twite pamoja na pacha wake
Mbutu Twite. Wasiwasi ulimuingia Twite lakini Yanga walimtumainisha na
kumuambia kuwa suala la kusaini timu mbili awaachie wao wanayanga.
Yanga waliishawishi APR kuwauza
wachezaji hao wawili Twite’s kwa timu yao ya zamani St Eloi Lupopo ya Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), na baadaye Yanga kuwanunua Twite’s kutoka St
Eloi Lupopo kwa majina yao ya kuzaliwa na si haya ya Bandia ambayo waliyapata
kwa ajili ya kupata uraia wa Rwanda… BAO
LA KISIGINO. Aidha Yanga wameshatia kibindoni Hati ya Uhamisho wa Kimataifa
(ITC) ya mchezaji huyo, kutoka Shirikisho la Soka (DRC), wakati Simba wanaendelea
kusubiri ITC ya mchezaji huyo kutoka FERWAFA, Shirikisho la Soka la Rwanda….BAO LA KICHWA.
Chama cha Soka Rwanda (FERWAFA) kimesema
"Hatuna taarifa zozote mpya kuhusiana na Mbuyu Twite kwenda Simba, Yanga
au kuondoka APR" alisema Katibu Mkuu wa FERWAFA, ndugu Michael Gasingwa.
Simba "Mbele ya mwenyekiti wetu Rage, viongozi wa FERWAFA na maofisa wa APR tulimsainisha Twite" alisema Kaburu.
Simba "Mbele ya mwenyekiti wetu Rage, viongozi wa FERWAFA na maofisa wa APR tulimsainisha Twite" alisema Kaburu.
Hivi ni lini wanazi wa mtashtuka kwamba mnachezewa akili na viongozi wenu? Hapo juu nani ni mwongo?? Halafu lawama mnazipeleka kwa Yanga
Mchezaji akisajiliwa inachukuliwa mpaka ITC yake sasa Kaburu na Rage waonyeshe angalau picha tu za kusaini mkataba na Twite achilia mbali mkataba wenyewe na ITC.
Muda ulioongezwa wa kufunga usajili
kutoka Agosti 10 hadi 15, mwaka huu na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
umeongeza wasiwasi na mashaka kwa Wanasimba kuongezwa huko kwa muda kuna lengo
la kuwaumiza wao.
No comments:
Post a Comment