BM BARBERSHOP KINONDONI

Saturday, August 18, 2012

SIJAWAHI KUMFUKUZA SHILOLE FLORA MVUNGI ALONGA

Habari hii nikwahisani ya Global Publishers:
STAA wa filamu za Kibongo, Flora Mvungi amekanusha madai ya kuwa aliwahi kumfukuza mwigizaji mwenzake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’. Tamko hilo limekuja mara baada ya Shilole ambaye sasa amejikita katika tasnia ya muziki kuachia wimbo wenye ujumbe unaosema Nyumba za Kupanga Lawama ambapo ilidaiwa kuwa alimuimbia Flora kwa kuwa waliwahi kuishi pamoja.

 “Mimi nilimpokea Shilole kipindi anatoka mkoa lakini baadaye nilimpa akili ya yeye kupanga kwake, sijamfukuza. Kama ameniimba mimi katika wimbo huo nitamshangaa,” alisema Frola ingawa kwa mujibu wa mtandao wa mmoja, Shilole alidai ameimba kwa kutoa ujumbe kwa jamii wala hakumlenga mtu.

1 comment:

  1. Umaarufu huu wa kupitia migongoni mwetu acheni pambaf nyie... Wewe Shilole kila siku wewe kila siku wewe huoni ni ujinga huo? Usipotajwa kuna kamdudu kanakuwasha nini? Tangaza kazi yako na imba kwa maendeleo yako. Halafu na wewe Flora bora siku hizi sikusikii sana lakini acha ubondi; pata mchumba olewa ushajichezea sana sasa unashuka thamani ndio muda wako wa kuolewa na kutulia nyumbanai; jifunze kwa wenzako kama Maimartha wa Shaa na wengineo... Tulieni nyie watoto mtyakuja juta baadae; umaarufu wa bongo huishia majuto waangalieni wenzenu. Mnatakiwa mkae na Bi Kidude awaelezee toka enzi za majahazi hadi leo kajifunza mengi yule dada mkubwa...

    ReplyDelete