MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC), Clement Mshana amewaomba radhi waumini wa dini ya
Kiislamu kwa kutoa takwimu zisizo sahihi, zinazohusu idadi ya waumini wa dini
ya Kiislam na Kikristo. Mshana aliomba radhi wakati akizungumza na waandishi wa
habari katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam jana.
Mshana alikiri kuwa, takwimu
zilizorushwa na kituo chake katika sherehe za Muungano mwaka huu hazikuwa
sahihi, hivyo na kwamba huo ndio msingi wa kuomba radhi. “Kipindi kilirushwa na
kituo chetu cha TBC kuhusiana na takwimu za idadi ya waumini wa Kiislamu,
Wakristo na dini nyingine zilikosewa,” alisema.
Alisema takwimu hizo zilichukuliwa kutoka katika mtandao wa WIKIPEDIA, ambazo zilionesha idadi ya Waislamu wakiwa asilimia 32, Wakristo asilimia 52 na dini nyingine asilimia 14. Alisema baada ya matangazo kurushwa hewani, walipokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa chama cha Tanzania, Muslim Professionals Association, Pazi Mwinyimvua. Mshana alisema, barua hiyo iliitaka TBC kujibu barua yao na kutaka ufafanuzi wa takwimu hizo na mahala walipozitoa. “Tulipokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Mei 15, mwaka huu ilioomba radhi waumini wa dini ya Kiislamu kwa kasoro hiyo iliyojitokeza” alisema Mshana.

Pia alisema licha ya kuomba
radhi, TBC ilitoa ufafanuzi juu ya takwimu zilizokosewa katika moja ya vikao
vya dini mjini Dodoma. Aidha Mshana aliwaomba waumini wa dini ya Kiislam
kujitokeza kwa wingi katika suala la sensa na kuhesabiwa, ili kupata takwimu za
watu katika Sensa hiyo itakayofanyika Agosti 26, mwaka huu.
Director General Clement Mshana
| ||
General Manager Bussiness Support: Joe Rugalabamu
|
General Manager Technical: Mr.Diotrefu Abenego
|
Director of Finance and Supply: Mr George Mziray
|
DHRA: Mrs. Joyceline Lugora
|
DOM: Mrs. Leocardian Rugimbana
|
DNCA: Mrs. Susan a God
|
Hiyo ndio matokeo ya kuajiri watu wasio weledi katika kazi. Kosa kama hilo halikustahili kufanyika. Pamoja na kuomba radhi TBC iwe macho na watu wanaoweza kupenyeza agenda mbaya kwa kusudi ili kufarakanisha jamii.
ReplyDelete