BM BARBERSHOP KINONDONI

Saturday, August 18, 2012

WAKANDARASI WA MIZIKI KUFANYA SHOO KWENYE WILAYA ZOTE TATU ZA DAR ES SALAAM WAKATI WA EID (Eid Mosi, Eid Pili na Eid Tatu)


Wajuzi wa Miziki ya Dansi wasio na Mpinzani Wakandarasi waja na SUPRISE wakati wa EID. Kesho Jumapili EID MOSI watakuwa TWANGA CITY Mango Garden Mchana kwenye Bonanza la Watoto kwa Kiingilio cha Shilingi 2,000/= kwa watoto na shilingi 5,000/= kwa wakubwa watakaowasindikiza watoto. Twanga haina Ubaguzi kila lika tunalijali (ITIFAKI IMEZINGATIWA).

Usiku ni burudani ya kukata na Mundu itakayoongozwa na Sura Mpya za Wacheza Shoo Mahili wakike waliokuwa Umangani na sasa wamerejea Kuongeza Nguvu ndani ya Bendi yao kwa Kiingilio cha Shilingi 8,000/= tu bila senti. Ukitoa BUKU KUMI unarudishiwa Chenchi ya Bia. Njoo upate RAP inayokamata ya NJEGERE MWENZIWE NI UBWABWA. huku Mirinda Nyeusi akiwa amepania kuudhihilishia ulimwengu kuwa yeye alizaliwa kwa ajili MUZIKI Siya kukosa hii Kitu. 
Katika kuhakikisha kuwa Burudani hii inawafikia wana Dar es Salaam wote Twanga Pepeta wazee wa Shamba La Twanga watahamia Wialaya ya Ialala siku ya Jumatatu wakati wa EID Pili katika Ukumbi Maarufu wa Dar West ulioko Tabata ili kuhakikisha watu wa pande ya Ilala wanalicheza Twanga.

Katika kuonyesha kuwa Twanga inawajali watu wake baada ya kuwamiss kwa muda Mrefu watahamia Wilaya ya Temeke siku ya Eid Tatu katika Ukumbi wa KOYAGA NIGHT PARK ulioko Kiwalani. Maonyesho haya yote yataanza Saa tatu kamili Usiku hadi Kijua kitakapotoka.

USIDANGANYIKE NJOO ULIKOZOEA

1 comment:

  1. Hongera kazi nzuri ya kutuhabarisha kuliko hata hao Twanga wenyewe big up sana kaka

    ReplyDelete