Vijana wa Kitanzania waliorejea
nyumbani Tanzania baada ya kuishi Ughaibuni kwa miongo mingi wameona ni vyema
wakashiriki na ndugu zao kwenye nchi waliyoizoea BONGO LAND baada ya kuimiss
kwa miaka kadhaa. Katika kuhakikisha kuwa hili linakuwa WABONGO HAWA WALIOREJEA
NYUMBANI TOKA KIWANJA wameandaa TUKIO la kihistoria na kulibatiza Jina la “BONGO
BACK 2 UK BASH” siku ya Jumamosi 25/08/2012 JOEVIC PUB Mbezi Beach jirani
kabisa na Mediterranean kwa Kiingilio cha Silingi 10,000/= Kabla ya Saa nne
Usiku na Shilingi 15,000/= baada ya saa nne. Viingilio vyote ni kwa pesa ya Kibongo
(Madafu). Kama una Dolali au UK Pound pia inakubalika. Njoo upate Miziki
Mchanganyiko pamoja na Jopo hili liliorejea Nyumbani KUWEKEZA.
BANGO LINAJIELEZA
VYEMA !!!!!!!!!!!!!!
No comments:
Post a Comment