BABA YANGU MZAZI MZEE ERNEST JUSTUS MUTTA |
WASIFU WA WAZAZI
Deo Mutta Mwantanga
ni Baba wa watoto watatu ambao amezaa na Jaquiline Ashery Mang’ara. Deo
alizaliwa miaka 42 iliyopita Mkoa wa Tanga Kijiji cha Msamaka Nazareth Wilaya
ya Korogwe tarehe 10/01/1970. Deo Mutta ni motto wa Kwanza kwenye Familia ya
Mzee Ernest Justus Stewart Mutta na mama Mary Paulo Mwambashi Shenyagwa ambao
walifunga ndoa yao mwaka 1967 na miaka mitatu baadaye walibahatika kupata motto
na kumuita Deo ambalo ni neon la Kilatini likiwa na maana ya MUNGU. Wakati huo
Mzee Mutta alikuwa ni Mfanyakazi wa Mamlaka ya Chai Tanzania Tawi la Mponde na
mama akiwa ni Nesi Hosiptali ya Bumbuli zote zikiwa Wilayani Lushoto Mkoa wa
Tanga
DEO MUTTA THOSE DAYS |
WASIFU WA KIELIMU KWA UFUPI
Deo alipata elimu
yake ya Msingi katika shule tofauti ndani ya Mkoa wa Tanga na baadaye Mkoani
Kagera ambako ndiyo chimbuko la Baba yake Mzazi ambaye sasa nimkazi wa kudumu
mjini Korogwe Mkoa wa Tanga. Shule alizosoma ndugu Deo ni pamoja na Nazareth Shule
ya awali Mwaka 1977-1979 Wilayani Korogwe Mkoa wa Tanga, Darasa la Kwanza nala
pili Shule ya Msingi Msamaka mwaka 1980-1981 Wilayani Korogwe Mkoa wa Tanga. Mwezi
Novemba Mwaka 1981 Baba yake Deo Mutta (Mzee Mutta) alipata uhamisho wa Kikazi
kwenda Mamlaka ya Chai Tanzania Tawi la Maruku Bukoba. Baada ya kufika Bukoba
Deo alijiunga na shule ya Msingi Bilele iliyoko Mkoani Kagera Wilaya ya Bukoba
Mjini Mwaka 1982-1985 darasa la tatu hadi lasita na baadaye alihamishiwa shule ya
Msingi Ibaraizibu iliyopo Mkoani Kagera Wilaya ya Bukoba Vijijini akiwa darasa
la Saba na kuhitimu elimu ya Msingi hapo mwaka Septemba, 1986.
Deo Mutta
alichaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari Bukoba
(Bukoba Secondary School) ambako alisoma kwa miezi sita tu yaani Januari 1987 hadi
Juni 1987 baada ya Baba yake kuhamishwa kikazi kwenda Mamlaka ya Chai Tanzania
Tawi la Rungwe Mkoani Mbeya. Deo alifuatana na Wazazi wake na kufanikiwa
kujiunga kwenye shule ya kulipia baada ya uhamisho wake kutoka Bukoba Sekondari
kuchelewa na kujiunga na Shule ya Sekondari Ndembela iliyopo Wilaya ya Rungwe
Mkoani Mbeya kilomita chache kutoka mjini Tukuyu na kudumu hapo kwa miaka mitatu
1987-1989 na kuhamia Shule ya Sekondari ya Irambo iliyopo Wilaya ya Mbeya
vijijini na kumaliza elimu ya Sekondari mwaka 1990 (Ordinary Level Education).
Deo mutta alijiunga
na elimu ya sekondari kwa ajili ya Kidato cha tano na sita mwaka 1991-1993
katika shule ya sekondari Mwakaleli Iliyoko Wilaya ya Rungwe na kumaliza elimu
ya Sekondari (Advanced Level Education). Baadaye alijiunga na Jeshi la Kujenga
Taifa kwa mujibu wa Sheria 1993-1994 Ruvu JKT 832 KJ. Deo alijiunga na Vyuo
mbalimbali ndani na nje ya Tanzania na kufanya vizuri kwenye Masomo yake.
MASUALA YA KAZI AJIRA
Deo Mutta pia
amefanya kazi kwenye Taasisi mbalimbali za Binafsi na Serikalini kwa vipindi
tofauti ikiwa ni pamoja na;
1. Mamlaka ya Chai Tanzania Tawi la Mponde Lushoto Tanga
2. Kalamu Stationaries – Korogwe Tanga
3. Muzdalifa Dispensary – Korogwe Tanga
4. Research International (RI - International) – Dar es Salaam
5. World Wide News Agency – Dar es Salaam
6. Steadman International – Dar es Salaam
7. Steadman Media Monitoring Agency – Dar es Salaam
8. Tanzania Conference Services LTD
9. Dar es Salaam City Council
10. Dar Rapid Transit – DART
11. Surface and Marine Transport Regulatory Authority – SUMATRA
12. Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania- UMATI
13. Tanzania National Road Agency - TANROADS
Familia
ya Deo Mutta
Mzee
Mutta alizaliwa 21/08/1947 na Mama Mutta 31/01/1950. Deo mutta ni mtoto wa
kwanza kati ya watoto sita kwenye familia ya Mzee Mutta. Mtiririko wa familia
kwa maana ya kuzaliwa nikama ifuatavyo:
The First Born Deo Mutta Birth Date 10/01/1970
Deo
Mutta anamke na watoto wane ambao ni pamoja na;
Pamoja
na familia ya Deo pia dada yake Rose Monica alibahatika kupata mume na kupata mtoto
anayejulikana kwa jina la Ernest Bahati Namanolo aliyezaliwa Mwaka 30/05/1997 Mdogo wake Filbert Mutta alipata
mke na kubahatika kupata motto wa kike anayeitwa Karen Filbert Mutta
aliyezaliwa mwaka 17/02/2010.
Ernest Bahati Namanolo - 30/05/1997
Karen Filbert Mutta - 17/02/2010
ANACHOPENDELEA
HOBBIES
Deo
Mutta anafani mbalimbali ikiwemo Mpira na ni mpenzi mkubwa wa miziki ya Dansi.
Katika historia ya Muziki alipata bahati ya kucheza mpira kwenye timu tofauti
tangu shule , Jeshini na Uraiani. Timu alizowahi kuchezea ni pamoja na;
1. Timu ya UMISHUMTA wilaya ya Bukoba Mjini
2. Timu ya UMISHUMTA wilaya ya Bukoba Vijijini
3. Timu ya Umishumta Mkoa wa Kagera
4. Timu ya Sekondari ya Ndembela Tukuyu
5. Timu ya Sekondari Irambo Mbeya
6. Timu ya Sekondari Mwakaleli Tukuyu
7. Timu ya UMISETA Wilaya ya Rungwe
8. Timu ya UMISETA Wilaya ya Mbeya
9. Timu ya UMISETA Mkoa wa Mbeya
10. Timu ya UMISETA Nyanda za Juu Kusini
11. Chai Sports Club Katumba
12. Kurugenzi Sports Club Tukuyu
13. Tukuyu Stras Wilaya ya Rungwe
14. MECCO Sports Club Mkoa wa Mbeya
15. MACHATA Sports Club – Lushoto
16. Nyota Sports Club – Korogwe
17. Manundu Shooting Stars – Korogwe
18. Ruvu Shooting Stars – Pwani
19. Mbezi Veteran – Dar es Salaam
Bwana
Deo Mutta ni mpenzi mkubwa wa Mpira na Shabiki wa Timu za
1. Real Madrid
2. Arsenal
3. Dar es Salaam Young Africans
Napenda
sana Muziki hususan muziki wa Dansi hususan Werrason kwa nje ya Tanzania na
Twanga Pepeta kwa Bendi za Kibongo ila anawaheshimu sana Msondo Ngoma Mambo
Hadharani.
ANACHOCHUKIA DEO MUTTA
Deo
kama binadamu wengine kuna mambo asiyoyapenda ila makubwa zaidi nihaya;
1. Hapendi wanafiki
2. Hapendi Wafitini
3. Hapendi wachonganishi
4. Hapendi wasiomcha Mungu
5. Anaichukia sana timu ya Simba Sports Club ya dare
s salaam Tanzania Mtaa wa Msimbazi.
KWA
UFUPI HUYO NDIYO DEO MUTTA MWANATANGA!!!!!!!
No comments:
Post a Comment