Kamati
ya utendaji ya klabu ya Yanga iliyokutana leo 05/08/2012 Makao makuu ya klabu
hiyo chini ya Mwenyekiti wake Yusufu Mehboob Manji imemtangaza Mheshimiwa
George Huruma Mkuchika kuwa mmoja wa wajumbe wa baraza la wadhamni wa klabu
hiyo. Sambamba na Mkuchika wengine waliochaguliwa ni pamoja na Seif Ahmed
Magari, Ammi Mpungwe, Isaack Chanji na Mohamed Nyengi amewateua kuingia katika
kamati ya utendaji huku jina moja likitafutwa kwa ajili ya kukamilisha idadi
kamili ya wajumbe wa kamati ya utendaji.
Uamuzi
huo umetolewa na mwenyekiti wa Yanga Yusufu Manji katika mkutano wa kusimikwa
rasmi madarakani kwa uongozi mpya wa klabu hiyo leo makao makuu ya klabu hiyo
chini ya mama mlezi wa Yanga mama Fatma Karume. Sambamba na uteuzi wa kamati
hiyo mpya ya utendaji, klabu hiyo pia imeamua kufutilia mbali kamati zote
ndogondogo ndani ya klabu hiyo kuanzia leo isipokuwa kamati ya uchaguzi
inayoongozwa na Mheshimiwa Jaji John Mkwawa.
Katika
kuhakikisha kunakuwepo na umoja zaidi ndani ya Yanga wakati wa maamuzi, uongozi
wa Yanga umesema utakuwa ukikutana na viongozi wa matawi kila mwezi kwa lengo
la kubadilishana mawazo. Katika mkutano wa kusimikwa kwa viongozi hao wapya wa
klabu viongozi wote wapya walikuwepo na kuapishwa na mwenyekiti wa baraza
la wazee Mzee Ibrahim Katundu isipokuwa mjumbe mmoja ndugu Abdalah
Bin Kleb ambaye yuko Kigali Rwanda akishughulikia masuala ya klabu ya Yanga. Katika
hatua nyingine mwenyekiti wa klabu hiyo Bwana Yusufu Manji amesema wanatarajia
kufanya sherehe ya kuchukua taji la Kagame baada ya mfungo wa mwezi wa Mtukufu
wa Ramadhani.
No comments:
Post a Comment