GLADYS
BOKESE
|
Katika
kujaribu kuziba pengo la nafasi ya mlinzi wa kati ambayo imeachwa na
mlinzi kitasa Kelvin Yondani maarufu kama VIDIC
aliyejiunga na klabu ya Yanga hivi karibuni, mabingwa wa bara Simba SC inakamilisha
usajili wa mlinzi wa timu ya taifa ya DRC Congo Gladys Bokese ambaye ni
mchezaji huru. Gladys Bokese ambaye alikuwa akiitumikia kwa mara ya mwisho
klabu ya Étoile Sportive du Sahel ya
Tunisia alitarajiwa kuwasili nchini Tanzania leo hii akitokea nchini Congo
tayari kukamilisha taratibu za usajili. Taarifa zilizoifikia Blog ya
Mwanatanga zimesema mchezaji huyo alikuwa apokelewe na Makamu Mwenyekiti wa
Simba Geofrey Nyange Kaburu uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere saa
10:00 jioni ya leo.
BOKESE
AKISHANGILIA GOLI
|
Gladys Bokese alizaliwa September
9, 1981 jijini Kinshasa ambako aliaanza kucheza soka akiwa na klabu
ya AS Bandal akicheza kama mshambuliaji. Toka Bandal alijiunga
na Daring Club Motema Pembe kifupi DC Motema Pembe akiwa na wachezaji
kadhaa nyota kama Mbala Mbuta Biscotte na Ngasanya Ilongo. Alianza kuichezea
timu ya taifa ya Congo mwaka 2006 na kuwa ni miongoni mwa wachezaji
waliounda kikosi kilichoshiriki fainali za mataifa ya Afrika mwaka huo. Alipojiunga
na timu ya taifa kocha wa timu ya taifa ya Congo Claude Le Roy
alimbadilisha nafasi ya uchezaji na kumtumia kama mlinzi wa kati eneo ambalo
amelimudu vema na mpaka sasa akiwa ni mlinzi wa kati tegemeo.
BOKESE
AKIWA KATIKA MAJUKUMU YA KITAIFA
Taarifa za uhakika za mchezaji huyo
kuja Tanzania zimethibitishwa na ndugu wa karibu wa mchezaji huyo ambaye
amekuwa na mahusiano mazuri na Blogger hii.
No comments:
Post a Comment