BM BARBERSHOP KINONDONI

Monday, August 6, 2012

UJENZI BARABARA YA MSATA KIWANGWA BAGAMOYO KIWANGO CHA LAMI KUKAMILIKA PUNDE

Ujenzi wa Barabara ya urefu wa Kilomita sitini na tano (65) kutoka Bagamoyo kupitia Kiwangwa hadi Msata yenye urefu wa kilomita 65 umekamilika kwa asilimia takribani 59.6% baada ya jumla ya kilomita 35 kukamilika kwa kiwango cha lami. Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS wanakusudia kutumia barabara hii kwa Magari yote ya Usafiri wa Umma yanayotokea Kanda ya Kaskazini kwa maana ya Mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Manyara na Arusha kutumia barabara hii pindi itakapokamilika ili kupunguza msongamano kwenye barabara ya Morogoro hususan pale Chalinze na Kibaha kwenye Mzani (Weight Bridge).
HUU NDIYO MUONEKANO WA BARABARA YA MSATA-KIWANGWA-BAGAMOYO KWA SASA
 Matarajio ya hivi karibuni ni kujenga kituo cha Mabasi kwa ajili ya Mabasi ya Mikoani eneo la Kunduchi yalipokuwepo Machimbo ya Kunduchi yaliyofungwa ili kuyafanya mabasi yanayotokea Kanda ya Kaskazini kuanzia Safari zake na kuishia kwenye Kituo hicho kipya pindi kitakapokamilika ili kupunguza msongamano katikati ya Jiji.
HAPA NI MJINI KIWANGWA ENEO MAARUFU KWA ULIMAJI WA MANANASI WILAYA YA BAGAMOYO MKOA WA PWANI

Mradi mwingine ni ujenzi wa barabara ya Bagamoyo Saadan Pangani hadi Tanga kwa Kiwango cha lami utakaoyawezesha mabasi yatokayo Tanga na Mombasa kupitia barabara hiyo ili kukuza utalii wa Mbuga pekee Duniani ambayo Wanyama huwa wanakwenda Beach (MBUGA YA SAADAN) ambayo inaambaa na Ukingo wa bahari kutokea Bagamoyo hadi Tanga. Kwa kufanya hivyo Mbuga hii itakuwa kwa kasi na kuwa kivutio kwa Watalii kuja kuona Maajabu hayo ya Dunia ya wanyama wanaoshinda Beach kupunga Upepo. Mradi huu wa Bagamoyo Saadan Pangani umeshaanza kutokea Muheza kwa kiwango cha lami na ujenzi unakwenda kwa Kasi ya kutia moyo.

BAADHI YA VIZUIZI VYA KUONYESHA TAHADHALI KWA WATUMIAJI WA BARABARA HIYO YA MSATA KIWANGWA BAGAMOYO WAKATI WA UJENZI KUEPUSHA AJALI

Sambamba na Mradi huu pia Wakala wa Barabara Tanzania unaendelea na ukarabati wa barabara ya Chalinze Segera Tanga ambao awamu ya kwanza iliishia eneo la Kitumbi Wilaya ya Handeni chini ya Kampuni ya Wachina na sasa ujenzi huo unaendelea kuanzia Kitumbi hadi Kwamichi Tanga chini ya Kampuni ya Kiisrael iitwayo SBI International. Ukarabati huu sasa unaendelea kwa kasi sana na unatarajiwa kukamilika katikati ya mwaka 1913.
WAJENZI KAZINI BARABARA YA MSATA KIWANGWA BAGAMOYO

Aidha ujenzi wa awamu ya kwanza wa kilomita 76 kuanzia Segera hadi Mkumbara kupitia vijiji na miji ya Segera Mashine, Chang'ombe, Mailikumi, Mandera, Kwakombo, Kwamdulu, Korogwe Mjini, Msambiazi, Mgobe, Nkhalekwa, Magila, Gereza, Kwasunga, Kwasunga Mpirani, Makuyuni, Madumu, Madala, Chepete, Chekelei, Mwisho wa Shamba, Mombo Mjini, Jitengeni, Kasiga, Mazinde, Mheza, , Kwenangu, Magila, Mkumbara, Goha, Manga, Mtindiro, Mkomazi na Bwiko. Mradi huu unajengwa na Kampuni ya STRABAG ambayo pia inajenga Barabara yenye urefu wa kilomita 21.9 ndani ya jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka-DART.
VIFAA VYA UJENZI VYA KISASA KWENYE BARABARA YA MSATA KIWANGWA BAGAMOYO

2 comments:

  1. Eeee mwanangu naona uko kwenye fani... hongera sana kwa kutangaza profession yako na mwajiri wako

    ReplyDelete