BM BARBERSHOP KINONDONI

Monday, August 6, 2012

MAMA KARUME AONGOZA JOPO LA YANGA KUWASILISHA KOMBE LA KAGAME MJENGONI LEO

MWENYEKITI WA YANGA AKIWA NA MAMA FATMA KARUME
 Kombe la Kagame limetinga Mjengoni muda mchache uliopita na kulitikisa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baada ya utambulisho uliofanywa na Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda. Alianza kwa kusema. “Tunao Wageni Mashuhuri walioiletea Sifa Nchi yetu kwa kutwaa Kombe la Afrika ya Mashariki na Kati Maarufu kama Kombe la Kagame mara mbili Mfululizo tena kwa KISHINDO siku chache zilizopita ndani ya Uwanja Mpya wa Taifa Pale Dar es Salaam ambao ni Timu ya YANGA. Timu hii imeongozwa na Mama yetu Mke wa Muasisi wa Muungano Mama yetu Bi. Fatma Karume Mama Karibu sana na nimefurahi kukuona ukiwa bado na afya tele. Pamoja na Mama Karume pia ameandamana na Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Yanga Eng. Francis Mponjoli Kifukwe (Makofi Mengi), Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Ndugu Yusuph Mehboob Manji (Makofi Mengi Sanaaaaaaaaaaaaaaa), Makamu Mwenyekiti Ndugu Clement Sanga (Makofi) pamoja na viongozi wengine waandamizi na Wazee wa Yanga wakiongozwa na Mzee Akilimali. Pia tunao wachezaji wote wa Yanga kama mnavyowaona wakiwa kwenye nguo zao zinazopendeza za Njano wote kwa ujumla simameni…. (Bunge lazizima kwa Ndelemo na Vifijo huku Captain wa timu hiyo Carnavaro ainua Kombe juu). Spika aliendelea najua Mheshimiwa Spika Mstaafu Samwel Sitta amenuna sana lakini hiyo ndiyo hali halisi na hata Simba wakija na kombe nitawatangaza… (Vicheko Bungeni)….. Tunawakaribisha sana na tunawatakia kila la kheri kwenye shughuli zenu za kuijenga klabu yenu ili mtuletee furaha zaidi siku zijazo jambo ambalo tunaimani linawezekana (Makofi mengi sanaaa na Sauti ya Mheshimia Nasari ilisikika kwa mbali ikisema Tano bila Kichekooooo na makofi ya kuipongeza Yanga yaliendelea na kumfanya Spika Acheke na kuwataka Wabunge kuwa watulivu ili shughuli nyingine ziendelee). 
Mama Fatma Karume
Baada ya Spika kukamilisha zoezi la kuikaribisha Yanga Mjengoni Spika alimuita Mheshimiwa Bernard Camilus Membe Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa awasilishe Hotuba yake. Katika utangulizi wake Mheshimiwa Membe alisema “Nimefurahishwa na Ujio wa Yanga humu ndani wakati wa Hotuba yangu kwakuwa name ni mdau mkubwa wa Timu ya Yanga Hongereni kwa ushindi wa Kagame (Makofi mengiii)” Mwisho wa kunukuu. Fuatana na www.mwanatanga.blogspot.com kwa habari zaidi na zakina muda mchache ujao kuhusu kutinga kwa Kombe la Kagame MJENGONI leo 06/08/2012.

No comments:

Post a Comment