Arsenal
inajitahidi kukamilisha utiaji saini wa makubaliano ya mkataba wa kudumu na
mchezaji Santi Cazorla kutoka klabu ya Malaga pamoja na mchezaji kiungo
mwenzake Nuri Sahin anayeingia kwa makubalino ya mkopo kutoka klabu ya Real
Madrid. Mpango wa kuhama kwa mchezaji wa Timu ya Taifa ya Uhispania Cazorla
mwenye umri wa miaka 27 kumekua na utata wa shida ya fedha inayoikumba klabu ya
Malaga hata hivyo anatazamiwa kupitia utaratibu wa afya wiki hii. Mchezaji
kiungo wa timu ya Taifa ya Uturuki mwenye umri wa miaka 23 Nuri Sahin atajiunga
na Arsenal chini ya mpango wa mkopo wa mwaka mmoja na Real Madrid. Lililobaki
ni baina ya mchezaji Sahin kukubaliana na klabu ya Arsenal juu ya malipo na
marupurupu. Kuna uwezekano mkubwa kwa wachezaji hawa kuhitimisha utaratibu huu
kabla ya msimu mpya kuanza.
Bado
Sahin hajapangiwa siku ya kufanyiwa majaribio ya afya. Arsenal inaanza msimu
mpya kwa pambano la ugenini dhidi ya Sunderland tarehe 18 Agosti 2012. Tayari
Gunners imewasajili wachezaji wawili mshambuliaji Lukas Podolski kutoka klabu
ya Cologne na mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud aliyekuwa akichezea klabu
ya Montpellier. Pamoja na hayo yote wingu zito bado limegubika majaliwa ya
nahodha Robin van Persie, ambaye ametamka kua hatoongezewa mkataba wake
unaomazika mwaka 2013.
Usajili wa wacheza kiungo Cazorla
pamoja na Sahin ingawa hakuna uhusiano na mizengwe ya Van Persie lakini
umechagizwa na habari kwamba mchezaji kiungo wa Arsenal Jack Wilshere hatoweza
kucheza kabla ya mwezi Oktoba kutokana na jeraha la goti.
Cazorla
aliyejiunga na Malaga kutoka klabu ya Villarreal mwaka mmoja tu uliopita ana
urefu wa futi 5 inchi 6 na ameichezea timu ya Taifa ya Uhispania mwaka 2008 na
kwenye mashindano ya Ulaya ya mwaka 2012. Sahin alisajiliwa na Real Madrid
kutoka Borussia Dortmund kwa mkataba wa miaka sita mnamo mwezi May 2011 lakini
ameshindwa kupata nafasi katika kikosi Mourinho ambapo kocha huyo ameweza
kumruhusu aondoke tu ila kwa mkopo.
No comments:
Post a Comment