BM BARBERSHOP KINONDONI

Wednesday, August 22, 2012

YANGA WATEMBELEA KUMBUKUMBU YA KUSIKITISHA YA MAUAJI YA KIMBARI MJINI KIGALI


Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji baada ya kupokewa na Kocha wa timu ya taifa ya Rwanda, Milutin Sredojevic 'Micho
MABINGWA wa Kagame Dar es Salaam Young African (Yanga) imewasili salama Kigali ikiongozwa na Mwenyekiti Yusuph Manji. Katika Uwanja wa Ndege Kigali Yanga walipkelewa na viongozi wa FERWAFA Pamoja na Kocha wa Timu ya Taifa ya Rwanda ambaye pia alishawahi kuifundisha Yanga Milutin Sredojevic 'Micho'. Yanga itakuwa Rwanda kwa siku kadhaa kwa ajili ya kambi yao ya kujiandaa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inayotarajiwa kuanza Septemba 15, mwaka huu.
Wachezaji wa Yanga wakitoka kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Rwanda Eneo la Remera Kanombe mjini Kigali, Rwanda
Timu ya Yanga mchana wa leo walitembelea makaburi ambayo walizikwa wahanga wa mauaji ya kutisha na kusikitisha ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994.Yanga ipo nchi humo kwa mwaliko wa Rais wa huko Paul Kagame aliyewaita kwa ajili ya kuwapongeza kutokana na kutwaa ubingwa wa Kagame katika michuano iliyofanyika nchini mwezi uliopita.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga Abdallah Binkleb alimesema kwamba  baada ya ziara hiyo, jioni wachezaji wa timu hiyo walifanya mazoezi katika uwanja wa Shirikisho la Soka la Rwanda (FERWAFA). Binkleb ameongeza kwamba, kesho watakwenda Ikulu kutimiza mwaliko wa Rais Kagame kabla ya Ijumaa kucheza na Rayon Sport na mchezo mwingine utakuwa siku ya Jumapili dhidi ya Polisi Rwanda.
Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji kulia akijadiliana na Kocha wa Yanga, Mbeligiji Tom Saintfiet na Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga
Wachezaji walioandamana na Timu ya  Yanga ni pamoja na;
Makipa; Yaw Berko, Ally Mustafa ‘Barthez’, Said Mohamed, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Juma Abdul, Oscar Joshua, David Luhende, Stephano Mwasika, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite, Ibrahim Job, Ladislaus Mbogo, Athuman Idd ‘Chuji’, Juma Seif ‘Kijiko’, Salum Telela, Nizar Khalfan, Shamte Ally, Idrisa Rashid, Omega Seme, Haruna Niyonzima, Rashid Gumbo, Nurdin Bakari, Said Bhanaunzi ‘Spider Man’, Hamisi Kiiza ‘Diego’, Didier Kavambagu, Jerry Tegete, Frank Domayo, Simon Msuva.

No comments:

Post a Comment