KIUNGO mchezeshaji wa Simba, Mrisho Khalfan Ngassa, amesema
makali aliyonayo mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Daniel Akuffor, ni tofauti na
wachezaji wengine aliowahi kucheza nao.
Akuffor, ambaye ni raia wa Ghana, amekuwa na mwanzo mzuri tangu asajiliwe na Wekundu hao ambapo amefanikiwa kufunga katika kila mchezo kwenye michezo mitatu Simba iliyocheza ikiwa Arusha.
Akizungumza na Championi Jumatano, Ngassa amesema amewahi
kucheza na washambuliaji John Bocco akiwa na Azam FC lakini pia Said Bahanuzi
katika kikosi cha Taifa Stars, lakini Akuffor ameonekana bora zaidi kwa upande
wake.
“Nafurahi sasa timu yetu tumeanza kuelewana katika safu ya
ushambuliaji na kwa upande wangu Akuffor namuona ni bora kati ya washambuliaji
ambao nimewahi kucheza nao kwa sababu, yeye ni mwepesi tofauti na washambuliaji
wengine,” alisema Ngassa. “Nimecheza naye katika michezo mitatu na ameonekana
ni mtu ambaye kwa beki mzembe ni rahisi kukufunga na nafurahi kuona na yeye
akifurahi kucheza na mimi timu moja, nadhani mashabiki wa Simba watulie, mambo
mazuri yanakuja.”
Safi sana;nilisema Ngasa ni proffessional na hachezi mpira kwa ushabiki ila kama kazi. Simba wanamtendea Ngasa vizuri sawa na wachezaji wengine kwa hivyo watarajie ushindi tupu licha ya wapinzani wao kuchagua kutumia umafia.
ReplyDelete