Usafiri
wa treni jijini Dar es salaam utaanza mwezi Oktoba baada ya kukamilika kwa
maboresho ya reli kutoka Ubungo hadi stesheni. Akizungumza jana baada ya
kufanya safari ya majaribio Naibu waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Dk. Charles
Tizeba alisema kufikia mwezi ujao treni hyo itaanza kubeba abiria ili kupunguza
matatizo ya usafiri kwa wakazi waishio maeneo inapopita treni hiyo.
“Kufika
Oktoba tutakuwa tumeanza kutoa huduma maana leo tumeangalia uwezekano na
tumeona tunaweza ufanya huduma na kurekebisha kasoro zilizobaki” alisema Dk
Tizeba .
Dk Tizeba
alisema kuwa reli hiyo kwa sasa bado haijakaa vizuri hivyo inahitaji
kurekebishwa ili treni hiyo iweze kwenda kasi zaidi. Kuna baadhi ya nyumba zitabolewa
kwa ajili ya usalama ili kuepusha madhara kwa siku za usoni hususan zile zilizojengwa
jirani na reli hiyo.
“Inashangaza
sana kwani kuna watu wamejenga nyumba zao jirani kabisa na reli na wengine
wamediliki kujenga mita moja kutoka relini, hii inahatarisha maisha yao wenyewe
na hata wasafiri watakaotumia treni” Hivyo alisema kuwa tayari watu hao
wametaarifiwa juu ya kuondoka katika maeneo hayo na kwamba watatakiwa kuvunja
wenyewe na wakikaidi basi watavunjiwa ili huduma hiyo ianze kutolewa mara moja.
No comments:
Post a Comment